IQNA

Mapambano ya Palestina

Mjumbe wa Jihad Islami apongeza uungaji mkono wa Iran kwa mapambano ya Wapalestina

22:15 - August 12, 2022
Habari ID: 3475612
TEHRAN(IQNA)- Mwakilishi wa harakati ya Jihad Islami ya kupigania ukombozi wa Palestina ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa uungajo mkono wake kwa taifa na harakai za mapamabo ya Palestina.

Akihutubia waumini wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran hii leo, Nasser Abu Sharif ameashiria historia ya mapambano (muqawama ) ya Wapalestina dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel na kuashiria kushindwa mtawalia utawala wa Kizayuni katika makabiliano na mkundi ya Palestina.

Amesema katika vita vilivyoanzishwa hivi karibuni dhidi ya Ukanda wa Gaza, harakati ya Jihadi Islami iliweza kuweka masharti yake kwa adui Mzayuni.

Amesema Jihadi Islami iliwea kuvurumisha mamia ya maroketi kuelekea maeneo yanayokaliwa kwa mabavu yaliyopachikwa jina la Israel ambapo harakati hiyo peke yake iliwalazimu Wazayuni kurudi nyuma na kukubali masharti ya kufikia usitishaji vita,.

Abu Sharif aliendelea kusema kuwa ushindi huo ulipatikana kutokana na uungaji mkono wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Ijumaa iliyopita Israel ilianzisha  mashambulizi yake makubwa ya mabomu huko Gaza, ambapo ililenga maeneo ya raia na kambi za wakimbizi. Jeshi la Israel lilidai lilikuwa likiwalenga wanachama wa Jihad, wakiwemo makamanda wakuu wa kundi hilo, lakini kulingana na maafisa wa Palestina, karibu nusu ya watu 44 waliokufa walikuwa raia wakiwemowatoto karibu 19

Takriban raia 350 wa Palestina pia walijeruhiwa.

Jihadi Islami  ilijibu jinai hiyo kwa kurusha mamia ya makombora kuelekea Israel na kuulazimisha utawala huo bandia kukubali kusimamisha mapigano.

Mapigano hayo yalikuwa mabaya zaidi katika Ukanda wa Gaza tangu vita vya siku 11 mwaka jana vilivyoua watu wasiopungua 250 katika eneo hilo la pwani na takriban watu 13 nchini Israel.

3480060

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha