IQNA

Umoja wa Wapalestina

OIC yapongeza mapatano ya makundi ya Palestina nchini Algeria

14:10 - October 16, 2022
Habari ID: 3475938
TEHRAN (IQNA) - Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imekaribisha tangazo la maridhiano na umoja wa kitaifa baina ya makundi ya Palestina, ambalo lilitiwa saini hivi karibuni nchini Algeria.

Sekretarieti ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu imetangaza katika taarifa yake kuwa: Hatua hii ni muhimu na chanya ya kumaliza hitilafu na kurejesha umoja wa kitaifa kati ya wananchi wa Palestina.

OIC pia imeishukuru serikali ya Algeria kwa kuwa mwenyeji wa mazungumzo kati ya makundi ya Wapalestina.

Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu pia imesisitiza kuwa inaunga mkono juhudi zote za kupatikana umoja wa kitaifa kati ya makundi ya Palestina.

Vyanzo vya habari vilitangaza Alhamisi iliyopita kwamba, makundi ya Wapalestina yametia saini "Azimio la Algeria la Umoja wa Kitaifa" mwishoni mwa mkutano uliofanyika nchini Algeria.

Taarifa iliyotolewa na makundi ya Wapalestina nchini Algeria imesisitiza umuhimu wa umoja wa kitaifa unaozingatia ushirikiano wa kisiasa kati ya makundi ya Palestina.

Miongoni mwa mambo yaliyotiliwa mkazo katika taarifa hiyo ni pamoja na kuimarisha nafasi ya Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) kama mwakilishi pekee wa kisheria wa wananchi wa Palestina, kuharakisha uchaguzi wa rais na wabunge katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ukiwemo mji wa Quds hadi mwaka mmoja baada ya kusainiwa kwa taarifa hiyo, kukomeshwa migawanyiko, kufanikishwa umoja wa kitaifa na ushirikiano wa kisiasa.

Makundi hayo ya kipalestina yaliyokutana nchini Algeria pia yamesisitiza haja ya kushikamana na mapambano ya wananchi na haki ya watu wa Palestina ya kupambana na Wazayuni maghasibu kwa njia mbalimbali.

3480870

Kishikizo: palestina aligiers
captcha