Munira Abdifatah Abd ambaye ni mwanafunzi wa katika chuo kimoja cha Qur'ani Tukufu mjini Nairobi alikuwa miongoni mwa kumi bora katika mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani ya Dubai mwaka huu ambapo alitunukiwa zawaidi ya ya takribani shilingi milioni mbili za Kenya. Binti huyo mwenye umri wa miaka 115 alikuwa wa nane kati ya washiriki 300 kutoka duniani kote, Mapmea mwaka huu pia katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani Munira alishiriki katika mashindano ya Qur'ani ya Msikiti wa Jamia mjini Nairobi ambapo alishika nafasi ya pili.
Katika mashindano hayo ya wanawake ya Kimataifa ya Qur’ani ya Sheikha Fatima Bint Mubarak yalioyofanyika hivi karibuni mjini Dubai washiriki wa bara la Afrika walishika nafasi za juu.
Aindati Sisi kutoka Senegal alinyakua nafasi ya kwanza huku Ayeshah Abubakr Hasan kutoka Nigeria na Shima Anfal Tabani kutoka Algeria akifuata.
Mashindano hayo yalihitimishwa Jumatano Tano Oktoba katika Jumuiya ya Utamaduni na Sayansi ya Dubai.
Hii hapa chini ni sehemu ya klipu ya Bi Munira akijibu maswalhi ya majaji katika mashindano hayo ya Qur'ani