IQNA

Qur'ani Tukufu Inasemaje /21

Mafundisho ya Qur'ani kuhusu utajiri, kuondoa umaskini

14:07 - October 20, 2022
Habari ID: 3475959
TEHRAN (IQNA) – Suala la umaskini limekuwa tatizo kubwa katika jamii za wanadamu katika historia. Je, mtazamo wa Uislamu ni upi kuhusu suluhisho la kimsingi la tatizo hili?

Kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu, bila ya mwanadamu kuwa makini kila mara kwa watu wanaomzunguka na kuwasaidia wenye mahitaji hakuwezi kuwa na matumaini ya kuondolewa maskini. Hili ni suala ambalo Qur'ani Tukufu inazungumza kwa upana.

Dhana iliyopewa jina la Infaq (kuwasaidia wanaohitaji) imeanzishwa kama suluhisho. Neno Infaq maana yake ni kujaza tundu na hapa linamaanisha kukidhi mahitaji ya kifedha. Ni aina ya sadaka katika Uislamu ambayo hutolewa bila ya matarajio yoyote ya malipo au fidia. Mtu hufanya Infaq kwa ajili ya kuboresha jamii na kumridhisha Mwenyezi Mungu.

Matokeo chanya ya Infaq sio siri. Miongoni mwayo ni kupunguza mapengo ya kijamii, kukuza ukarimu na huruma, kuongezeka kwa roho ya ukarimu, na zaidi ya yote, kumkaribia Mwenyezi Mungu.

Mafundisho haya yametajwa katika aya nyingi za Qur'ani Tukufu, ikiwemo katika aya ya 274 ya Surah Al-Baqarah:

" Wale wanao toa mali zao usiku na mchana, kwa siri na dhaahiri, wana ujira wao kwa Mola wao Mlezi; wala haitakuwa khofu juu yao, wala hawatahuzunika."

Hii inajulikana kama Aya ya Infaq na inatoa habari njema ya Mwenyezi Mungu kwa wale wanaofanya Infaq katika hali yoyote ile. Watu kama hao hawaogopi kupata umasikini wala kuhuzunika kwa sababu wanaamini ukweli wa ahadi za Mwenyezi Mungu na pia wanatilia maanani radhi za Mwenyezi Mungu na malipo ya Infaq ambayo watayapata huko Akhera.

Katika Tafsiri yake ya Noor ya Quran, Hujjatul Islam Mohsen Qara’ati anasema aya hii inajumlisha mafundisho ya aya 14 zilizotangulia zilizozungumzia Infaq.

Ni muhimu kutambua kwamba umuhimu unaohusishwa na Infaq katika Uislamu haumaanishi kuwa dini inahimiza kuomba, kwani katika Hadithi nyingi hatua kuwaomba wengine msaada wa kifedha bila ya haja imekuwa ikikosolewa. Pia aina bora ya Infaq ni kumpa mtu njia ya kuanza kazi ili kupata pesa badala ya kuwapa pesa.

Ujumbe wa Aya ya 274 ya Surat al-Baqarah:

1- Ni muhimu kuwa na moyo wa ukarimu na Infaq sio tu wakati mwingine kutoa pesa kwa masikini. Neno Yunfequn linamaanisha kuendelea kwa Infaq.

2- Hakika Aya inaonyesha jinsi Infaq ilivyo na ujira mkubwa: (wana ujira wao kwa Mola wao Mlez).

3- Ahadi za Mwenyezi Mungu ni himizo lililo bora zaidi kwa wanadamu kutenda mema.

4- Kuhisi amani na usalama ni miongoni mwa neema zinazokuja na Infaq: (hakutakuwa na khofu juu yao, wala hawatahuzunika).

Kwa mujibu wa wafasiri wengi wa Qurani, mfano sahihi wa kufanya Infaq ambayo aya hii inarejelea ni Imam Ali ibn Abi Talib (AS) na kwamba aya hii imeteremka baada ya Infaq yake.

Allamah Tabatabai, katika Tafsiri yake ya Qur'ani Tukufu ya Al-Mizan, anataja orodha ndefu ya tafsiri za Quran na vitabu vya Kiislamu ambavyo vimesimulia kisa cha Infaq hiyo.

Imam Ali (AS) alikuwa na Dirham nne. Alitoa yote kama Infaq, Dirham moja usiku, moja mchana, moja kwa faragha na moja hadharani.

captcha