IQNA

Qur'ani Tukufu inasemaje / 20

Qur'ani Tukufu inahimiza mazungumzo

12:37 - July 30, 2022
Habari ID: 3475556
TEHRAN (IQNA) - Mhadhiri mmoja wa Kiislamu ameashiria aya kadhaa za Qur’ani, ili kubainisha kwamba Qur’ani Tukufu imeweka msingi wa kuanzisha mahusiano na mazungumzo.

Profesa Rasul Rasulipour, mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Kharazmi nchini Iran, alisema hayo katika semina. Ifuatayo ni sehemu ya hotuba yake.

Mada ambayo nimeichagua ni mwaliko wa Qur'ani Tukufu wa kuelekea kwenye mazungumzo. " Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lilio sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala tusifanyane sisi kwa sisi kuwa Waola Walezi badala ya Mwenyezi Mungu..." (Surah Al-Imran, aya ya 64)

Maandiko ya kidini kidhahiri huwa yanaonekana kama yasiyohimiza mazungumzo kwa mtazamo wa juu juu, hata hivyo, nataka kupinga maoni haya na kusema kwamba Uislamu unahimiza mazungumzo bila masharti.

Baadhi ya aya za Quran zinazokuza mazungumzo

Katika Qur'ani Tukufu mara kadhaa kauli ya “yas’alunak” inayomaanisha “Wanakuuliza wewe [Mtume]”. Maswali haya na majibu ya Mtume Muhammad (SAW) kwao yanaonyesha msururu maalumu wa maandiko matakatifu na hivyo tunapaswa kujifunza kutokana na kauli hizo.

Au aya ya 6 ya Surah Fussilat isemayo “ Sema: Hakika mimi ni mtu kama nyinyi; inafunuliwa kwangu ya kwamba Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu. Basi nyookeni sawa kumwendea Yeye, na mumtake msamaha, na ole wao wanao mshirikisha,"

Aya hii na zinginezo kama hii zinatayarisha mazingira ya mazungumzo na Mtume (SAW) kwani watu wanaona kwamba licha ya uzoefu wake mwingi kuhusiana na Mwenyezi Mungu, Mtume Muhammad (SAW) pia alionyesha kuwa hakuwa anafahamu hatima yake.

Ni dhahiri kwamba kuzingatia umuhimu wa mafundisho ya kidini kutapelekea kuangazia mafundisho yanayorejelea ubora na uhalali wa dini hiyo. Hata hivyo, Mwenyezi Mungu anasema “Si kwa matamanio yenu, wala matamanio ya Watu wa Kitabu! Anaye fanya ubaya atalipwa kwalo, wala hatajipatia mlinzi wala wa kumnusuru, isipo kuwa Mwenyezi Mungu.” (Surah An-Nisa, aya ya 123).

Kwa hiyo, kwa mujibu wa Qur'ani, kinachobeba umuhimu ni matendo yetu.

Kuhusu uwezekano wa kushiriki katika mazungumzo kwa njia maandiko matakatifu mtu anaweza pia kurejelea aya ya 24 na 25 za Surah Saba: “Sema: Ni nani anaye kuruzukuni kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Sema: Mwenyezi Mungu! Na hakika sisi au nyinyi bila ya shaka tuko kwenye uwongofu au upotofu ulio wazi.  Sema: Nyinyi hamtaulizwa kwa makosa tuliyo yafanya, wala sisi hatutaulizwa kwa mnayo yatenda nyinyi."

Habari zinazohusiana
captcha