IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran

Mustakabali wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran umeng'ara zaidi

19:58 - October 21, 2022
Habari ID: 3475967
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema mustakabali wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran hii leo umeng'ara zaidi kuliko wakati wowote ule.

Akihutubia waumini walioshiriki Sala ya Ijumaa hii leo hapa mjini Tehran, Ayatullah Ahmad Khatami amesema Idara ya Mahakama ya Iran inapaswa kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wafanya fujo na ghasia hapa nchini. 

Amewataja wafanya fujo hao kama wasaliti wa taifa, ambao wanafuata mdundo wa ngoma inayopigwa na maadui wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Ayatullah Khatami ameashiria mustakabali wa mafanikio wa Mapinduzi ya Kiislamu na kueleza kuwa, "Katika miaka ya karibuni, maadui wamekuwa na ndoto nyingi dhidi ya taifa la Iran, lakini ndoto hizo hazikuambulia chochote, na mustakabali wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran hii leo umeng'ara zaidi kuliko huko nyuma."

Ayatullah Khatami amesema madola ya kibeberu na kiistikbari duniani yakiongozwa na Marekani yanapinga Uislamu halisi wa Mtume Muhammad SAW. Ameendelea kusema kuwa, madola hayo ya kibeberu hayapendezwi hata kidogo na Uislamu ulioko katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kaimu Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran ameeleza bayana kuwa: "Ili kuweza kuzishinda njama tarajiwa za maadui, lazima tujiandae na kuwa tayari katika nyuga za siasa, usalama, utamaduni na uchumi."

Ayatullah Ahmad Khatami  amesisitiza kuwa, njia mbili kuu za kusambaratisha na kuibuka mshindi mkabala wa njama hizo za maadui ni kupitia muqawama (mapambano) na subira.

Kwingineko katika hotuba yake, Ayatullah Khatami ameashiria stratejia ya kujihami ya Iran na kubainisha kuwa, "Katika miaka ya hivi karibuni, Jamhuri ya Kiislamu haijaishambulia nchi yoyote, lakini imechukua hatua za kujilinda."

4093345

captcha