IQNA

Dini

Rais wa Iran akutana na Wakristo Wairani katika mkesha wa Krismasi

21:00 - December 25, 2024
Habari ID: 3479953
IQNA - Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutana na baadhi ya Wakristo wa Iran Jumanne jioni.

Amewapongeza Wakristo wote duniani kwa mnasaba wa sikukuu ya Krismasi na akaelezea matumaini ya kupatikana amani, usalama na wema kwa watu duniani kote.

Rais, akirejelea mafundisho ya Qur'ani Tukufu ambayo yanaeleza kwamba hakuna tofauti kati ya Mitume wa Mwenyezi Mungu, alisisitiza kwamba "tunanyenyekea kwa yale ambayo Mitume wote walilingania".

Ameongeza kuwa, "hii ni imani ambayo Mwenyezi Mungu ametuteremshia ndani ya Qur'ani Tukufu."

Rais Pezeshkian alifafanua zaidi juu ya falsafa ya kutuma manabii, akisema kwamba Qur'ani Tukufu inasema watu wote waliwahi kuwa umma moja, na Mwenyezi Mungu aliwatuma mitume kuleta habari njema na kutoa mwongozo.

Mwenyezi Mungu aliwapa maandiko kufanya kazi kwa msingi wa haki katika jamii na kusuluhisha mabishano, alibainisha.

Rais wa Iran alirejelea mazungumzo kati ya Nabii Isa Masih yaani Yesu (AS) na Wayahudi katika Qur'ani Tukufu, akibainisha kwamba Yesu anasema kwamba "Mungu ni Mungu wetu na Mungu wenu, na tunapaswa kumwabudu Mungu mmoja."

Alisema ni lazima watu wote wafuate njia hii, akiongeza kwamba ikiwa kila mtu ataifuata na kukumbatia ukweli, haki, na uadilifu, ni tofauti gani ambazo watu wanaweza kuwa nazo wao kwa wao?

Rais Pezeshkian amesisitiza kwamba migogoro yote inatokana na ubinafsi wa mtu mmoja-mmoja, na huku akisisitiza kuwa wanadamu wana chimbuko moja amesema: "Mwenyezi Mungu anasema kwamba lugha, jinsia, na kabila au kaumu si mambo ya kubainisha ubora kwani ubora kwake ni ni wa wale walio wema zaidi na wakweli. Yeyote aliye mwema na muadilifu zaidi ndiye aliye bora mbele ya Mwenyezi Mungu.

3491203

Habari zinazohusiana
Kishikizo: krismasi rais wa iran
captcha