IQNA

Mashahidi wa Muqawama

Qari wa Misri asoma Qur'ani Tukufu katika hauli ya mashahidi wa Muqawama

15:37 - January 01, 2023
Habari ID: 3476341
TEHRAN (IQNA) – Hauli imefanyika mjini Tiro nchini Lebanon kwa ajili ya makamanda wa muqawama mashahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani na Abu Mahdi al-Muhandis.

Kituo cha Imam Hussein (AS) cha mjini Tiro kiliandaa hafla hiyo kabla ya mwaka wa tatu wa kuuawa shahidi makamanda hao.

Ilihudhuriwa na watu mashuhuri wa kidini kama Sheikh Ali Arif na Hajj Bilal Daghir pamoja na maafisa kadhaa wa Hizbullah.

Maqari kadhaa, akiwemo Abdul Rahman al-Khouli kutoka Misri na Mohammad Ghalmoush kutoka Lebanon, walikariri aya za Qur'ani Tukufu katika ibada hiyo ya kumbukumbu.

Pia iliangazia hotuba za watoto kadhaa wa mashahidi wa Hizbullah na kuonyeshwa klipu ya video kuhusu Jenerali Soleimani.

Lt. Jenerali Soleimani, ambaye alikuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Naibu Kamanda Jeshi la Kujitolea la Wannachi wa Iraq (PMU) Abu Mahdi al-Muhandis, na wanamapambano wenzao waliuawa katika shambulio la ndege zisizo na rubani za Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad mapema  Januari 3, 2020. Shahidi Soleimani alikuwa ameelekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa serikali ya nchi hiyo.

Ikulu ya White House na Pentagon ilitangaza kuwa ilihusika na mauaji hayo ya kigaidi  na kuthibitisha kuwa shambulio hilo lilitekelezwa kwa maelekezo ya Rais wa Marekani wa wakati huo Donald Trump.

Mipango mbalimbali imepangwa kuandaliwa nchini Iran, Iraq na nchi nyingine kadhaa ili kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha kishahidi cha Jenerali Soleimani, al-Muhandi na wanajihadi wenzao.

Egyptian Qari Recites Quran in Memorial Service for Martyrs Soleimani, Al-Muhandis

Egyptian Qari Recites Quran in Memorial Service for Martyrs Soleimani, Al-Muhandis

4111031

captcha