IQNA

Wasomaji maarufu wa Qur'ani Tukufu / 11

Qiraa ya kipekee ya Muhammad Abdul Aziz Hassan

20:49 - November 20, 2022
Habari ID: 3476120
TEHRAN (IQNA) – Qarii mashuhuri wa Misri Muhammad Abdul Aziz Hassan alikuwa na umahiri wa kipekee katika ustadi wa usomaji (qiraa) Qur’ani ambapo baadhi ya wataalamu wanasema wasikilizaji wanahisi kuwa Qur’ani inateremshwa kwao wanaposikiliza kisomo cha Ustadh Hassan.

Msikilizaji anaweza kuona kwa uwazi kipaji cha Ustadh Hassan anaposikiliza kisomo chake. Kazi zake zina hadhi ya juu katika nyanja za kihisia.

Ustadh Hassan ana vigezo vyote vya usomaji mzuri. Hii ina maana kwamba kazi zake ni za kitaalamu huku pia zikiwapa wasikilizaji uzoefu mzuri wa kihisia.

Moja ya nukta kuu kuhusu kisomo chake ni kwamba ana mtindo tofauti kwa kiasi fulani ikilinganishwa na wasomaji wengine. Hakuna usomaji mwingine unaofanana na ule unaofanywa na Ustadh Hassan.

Baadhi ya wataalamu wanasema kazi za Mwalimu Abdulfattah Sha'shaei zinakaribiana na mtindo wa Ustadh Hassan.

Usomaji wa Ustadh Hassan ni wa kiufundi sana hivi kwamba mtaalam wa qiraa anaweza kufikiria kuwa haiwezekani kuwa na kazi kamili zaidi yake.

Moja ya sababu za ubora wa qiraa yake ni kwamba alikuwa na uwezo kamili kuhusu Saut na Lahn.

Kuelewa Saut katika usomaji Qur’ani ni muhimu sana kwa qari kwani humwezesha wasomaji bingwa kama Ustadh Hassan kuendelea na usomaji wa Qur’ani kwa masaa mawili huku akihifadhi ubora wa usomaji.

Kuiga usomaji wake ni kazi ngumu lakini ni jambo linalowezekana. Ustadh Hassan alikuwa na mpango maalumu kwa kila neno la Qur’ani  alilotamka. Kwa hivyo, sifa nyingine ya kazi yake ni umakini wake kwa undani.

Kwa upande mwingine, qarii  huyu maarufu wa Misri alikuwa na uwezo kamili juu ya Waqf na Ibtida (kutulia na kuanza upya). Hata mwanafunzi mmoja wa Saudia ameandika makala ya Shahada ya Uzamivu au Ph.D. imeandikwa kwa msingi wa mbinu ya  Waqf na Ibtida ya  Ustadh Hassan

Hapa chini ni klipu ya Ustadh Muhammad Abdul Aziz Hassan akisema aya za Sura Al-Ghafir.

captcha