IQNA

Wasomaji Maarufu wa Qur'ani Tukufu /6

Kamil Yusuf; Qari aliyeanzisha mtindo wake kwa kusikiliza visomo vya wengine

13:51 - November 03, 2022
Habari ID: 3476029
TEHRAN (IQNA) – Mmoja wa wasomaji maarufu wa Qur'ani Tukufu nchini Misri ambaye aliweza kuendeleza mtindo wake wa usomaji kwa kuwasikiliza tu wasomaji wakubwa alikuwa Sheikh Kamil Yusuf Al-Bahtimi.

Alipata ilhamu kutoka wasomaji wakubwa wa Qur'ani Tukufu kama Sheikh Muhammad Rif’at na naye pia akawapa ilhamu wasomaji wa Qur’ani baada yake.

Kamil Yusuf alizaliwa mwaka wa 1922 katika kijiji cha Sheikh Bahtim. Baba yake, ambaye alikuwa mmoja wa wasomaji wa kijiji hicho, alimtambulisha kwenye ulimwengu wa usomaji wa Qur'ani Tukufu katika umri mdogo.

Kamil alihifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu akiwa na umri wa miaka kumi. Pia alijifunza Adhana (mwito wa kusali).

Mwanzoni muadhini wa msikiti wa kijiji hicho hakumruhusu kuadhini kwa sababu alimuona kuwa mdogo sana. Walakini, baada ya kuadhini kwa uzuri na wote kuthibitisha talanta zake, muadhini mkuu alikubali.

Katika miaka yake ya mapema ya ujana, Sheikh Kamil alianza kusikiliza visomo vya Qur'ani vya Ustadh Muhammad al-Sayfi na kuiga mtindo wake.

Al-Sayfi punde si punde alitambua kipawa cha Kamil na akamchukua mvulana huyo mdogo kwenda naye katika miji tofauti ya Misri, ikiwa ni pamoja na Cairo, kusoma Kurani.

Kamil pia alijaribu kufaidika na mitindo ya kisomo ya Sheikh Muhammad Rif’at na Sheikh Muhammad Salamah. Punde si punde alijulikana kama qari mkubwa kote Misri.

Ni muhimu kutambua kwamba wasomaji wa Qur'ani Tukufu ambao ni mashuhuri katika zama Misri walikuwa wamejifunza usomaji wa Qur'ani kwa kuhudhuria madarasa maalumu za Qur'ani lakini Kamil Yusuf alianzisha mtindo wake kwa kusikiliza tu visomo vya Qur'ani vya wasomaji wengine.

Kamil Yusuf aliaga dunia na kurejea kwa Mola Wake mnamo Februari 6, 1969.

3481061

captcha