IQNA

Wasomaji maarufu wa Qur'ani Tukufu / 2

Sheikh Rafaat; Mtaalamu wa Usomaji wa Qur'an kwa msingi wa maana

17:56 - September 11, 2022
Habari ID: 3475768
TEHRAN (IQNA) – Sheikh Muhammad Mahmood Rafaat alikuwa miongoni mwa wasomaji Qur'ani mahiri nchini Misri. Ingawa alikuwa na ulemavu wa macho, aliibua kwa namna fulani mtindo tofauti wa qiraa au usomaji Qur'ani ikilinganishwa na maqari au wasomaji wenzake kwa kutumia silika na hisia zake za kina.

Rafaat (1882-1950) alizaliwa Cairo na alipoteza uwezo wake wa kuona kabla ya kufikisha miaka 6 kutokana na ugonjwa. Ugonjwa huu ulikuwa hatua ya mabadiliko katika maisha yake. Kuna vipofu kadhaa miongoni mwa makari mahiri wa Misri akiwemo Sheikh Muhammed Abdulaziz Hasan, Mohamed Omran, Mahmood Ramadan, na Muhammad Mahmood Rafaat. Mbali na nukta za kiufundi za usomaji wakati kuchunguza kazi za wasomaji hao pia mtindo wao wa usomaji wenye hisia maalum za kiroho na hii ni mashuhuri zaidi katika kazi za Sheikh Rafaat.

Rafaat aliweza kuihifadhi Qur'an yote kikamilifu akiwa bado mtoto kutokana na kutiwa moyo na baba yake. Sheikh Ali Mahmood (1878-1943) alisikia kisomo cha Rafaat na aliguswa nacho. Alisema basi kwamba mustakabali mzuri ulikuwa unamngojea mtoto huyo kwani angekuwa qari mkubwa kote ulimwenguni, na utabiri wake ulitimia.

Maisha ya kikazi ya Sheikh Rafaat yanaweza kuwekwa katika vipindi viwili; cha  kwanza kinahusiana na miaka hadi alipofikisha umri wa miaka 32. Katika kipindi hiki, hakuna maikrofoni yoyote ambayo ilikuwa yakitumiwa katika vikao vya Qur'ani na wasomaji waliokuwa na sauti yenye nguvu zaidi walizingatiwa zaidi kwani wangeweza kusoma mbele ya idadi kubwa ya watu. Hata hivyo, katika kipindi kilichofuata, ambacho ni baada ya kufikisha umri wa miaka 32, vipaza sauti viliingia katika duru za Qur'ani. Hii ilipelekea wengi Misri na dunia nzima kuweza kubaini na kupendezwa na usomaji wa Rafaat.

Miongoni mwa sifa muhimu zaidi za usomaji wa Rafaat ni hali yake kiroho na ubunifu ambao wake ulikuwa nadra miongoni mwa wasomaji wengine wa Qur'ani Tukuf . Mtu anaweza kusema kwamba kisomo chake kina msingi wa maana; ina maana kwamba hata wale wasiojua Kiarabu wanaathiriwa na jinsi Rafaat alivyosoma aya kwa hisia.

 Makala haya yalikuwa ni mukhtasari wa matamshi yaliyotolewa na Hamidreza Nasiri, qari wa kimataifa wa Iran, katika mahojiano na IQNA.

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha