IQNA

Wasomaji Maarufu wa Qur'ani Tukufu /1

Mahmud Ali Al-Banna, Qari aliyetumia maisha yake kutumikia Qur'ani (Video)

11:36 - September 06, 2022
Habari ID: 3475742
TEHRAN (IQNA) – Qari wa Misri Mahmud Ali Al-Banna (1926-1985) alikuwa miongoni mwa wasomaji mashuhuri wa Qur'ani wa zama zake.

Alizaliwa Desemba 1926 katika kijiji kiitwacho Shibra katika Jimbo la Menofia la Misri. Baba yake alikuwa mkulima.

Mahmoud alianza kujifunza Qur'ani kwa moyo au kuhifadhi akiwa na umri wa miaka sita katika Shule ya Ahmadi ya kijiji hicho.

Kila usiku alikuwa akipitia yale ambayo tayari alikuwa amehifadhi pamoja na aya ambazo mwalimu wake alikuwa anamtaka kuzisoma siku iliyofuata.

Mwalimu wake na watu kama yeye katika vijiji kote Misri walitoa mchango mkubwa katika kuendeleza kuhifadhi na kusoma Qur'ani nchini humo na kutoa mafunzo kwa watu kama al-Banna.

Mahmoud al-Banna anasema mara moja mwalimu wake alimwadhibu ingawa alikuwa amefanya vyema katika usomaji wake.

“Nilirudi nyumbani huku nikilia, nikamweleza mama yangu kilichotokea. Mama yangu alisema alimwomba mwalimu aniadhibu kwa sababu alihisi sikuwa na umakini unaohitajika wakati wa kujifunza Qur'ani.”

Mahmoud al-Banna alikuwa mtu wa dini sana na alitumia maisha yake yote katika kuitumikia Qur'ani Tukufu. Mwanawe Ahmed amefuata nyayo za baba yake na sasa ni msomaji mzuri wa Qur'ani.

Anasema kwamba baada ya kifo cha baba yake, mama yake alimwambia ajifunze kusoma Quran.

“Nilikuwa mfanyabiashara na sikufikiria kuwa qari. Usiku huo niliota ndoto ambayo nilianguka kisimani na kuanza kulia. Baba alikuja na kunishika mkono na kunitoa kisimani. Mama yangu aliota ndoto usiku uleule ambapo baba yangu alimpa mashati mawili na kumwambia anipe moja kati ya hizo. Hilo lilinitia moyo kuanza kujifunza usomaji wa Qur'an.”

captcha