IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Wahifadhi 173 kutoka nchi 123 wanashiriki mashindano ya Qur'ani ya Makka

18:15 - August 11, 2024
Habari ID: 3479264
IQNA - Jumla ya washiriki 173 kutoka nchi 123 wanashiriki katika toleo la 44 la Mashindano ya Kimataifa ya Mfalme Abdulaziz ya Kuhifadhi , Kusoma na Kutafsiri Qur'ani Tukufu huko Makka.

Waziri wa Masuala ya Kiislamu wa Saudi Arabia ambaye pia ni Msimamizi Mkuu wa mashindano hayo Abdullatif bin Abdulaziz Al-Sheikh alizindua hafla hiyo Jumamosi.

Akizungumza katika ufunguzi wa hafla hiyo, Al-Sheikh aliwakaribisha washindani hao na kusema kuwa Wizara imepata heshima kubwa kufanya hafla hii ambayo inashuhudia ushindani baina ya Waislamu na kuimarisha kushikamana kwa vijana na Quran Tukufu.

 “Wizara imekuwa ikitaka shindano hili liwe katika viwango vya juu na hatua zimechukuliwa ili kuwe na jopo la majaji wanaozingatia haki na uwazi,” alisema na kuongeza kuwa “mwaka huu, jopo la majaji lina  wasomi wenye ujuzi. na uzoefu kutoka Saudi Arabia, Jordan, Mali, na Pakistan.”

Aidha alisema kuwa shindano la sasa limeshuhudia idadi kubwa ya washiriki tangu lilipoanzishwa, mwaka 1978.

Mwenyekiti wa jopo la majaji Dk.Fahd bin Faraj Al-Juhani, alitoa hotuba ambapo alisema kuwa teknolojia ya kisasa itatumika katika tathmini yao.

3489450

Habari zinazohusiana
captcha