IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Washindi wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Makka wazawadiwa

14:46 - August 23, 2024
Habari ID: 3479318
IQNA - Wakati wa hafla katika Msikiti Mkuu wa Makkah, washindi wa Mashindano ya 44 ya Kimataifa ya Mfalme Abdulaziz ya Kuhifadhi, Kusoma na Kutafsiri Qur'ani wametangazwa na kutunukiwa zawadi.

Hafla ya kufunga mashindano hayo ilifanyika Jumatano jioni ambapo washindani wakuu katika kategoria tano za walitambulishwa.

Anas bin Ateeque kutoka Bangladesh alikuja wa kwanza katika kuhifadhi Qu'rani Tukufu kikamilifu, na kushinda zawadi ya pesa taslimu ya riyal za Saudia 200,000.

Mshindi wa pili katika kitengo hiki alikuwa Mazhir Yabtu wa Ufilipino, huku wawakilishi wa Libya, Yemen na Mali wakiibuka wa tatu hadi wa tano mtawalia.

Katika kundi la kuhifadhi Juzuu 15 (nusu ya Qur'ani), Muaz Mahmud kutoka Bangladesh alishinda zawadi ya kwanza, akifuatiwa na Obada Nouraldin Mohammed kutoka Palestina na Ahmed Farhan kutoka Indonesia.

Mahufadh kutoka Mali na Marekani walishika nafasi ya nne na ya tano katika kitengo hiki, mtawalia.

Wawakilishi wa Iran katika mashindano hayo, Mohammad Hossein Behzadfar na Mohammad Mehdi Rezaei, hawakuwa miongoni mwa washindani watano bora katika makundi hayo mawili.

Jumla ya washiriki 174 kutoka nchi 123 walishiriki katika duru ya mwisho mashindano hayo ya kimataifa la Qur'ani ambayo yalifanyika katika Msikiti Mkuu wa Makka kati ya Safar 5 na 17, 1446 AH (Agosti 9 na 21, 2024)

 

.

3489608

captcha