IQNA

Maonyesho ya Qur'ani

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu kufanyika Karbala, Iraq

11:29 - January 06, 2023
Habari ID: 3476364
TEHRAN (IQNA) – Mji mtakatifu wa Karbala nchini Iraq utakuwa mwenyeji wa awamu ya pili ya Maonyesho ya kimataifa ya Qur’ani Tukufu ndani ya wiki chache kuanzia sasa.

Maoneysho hayo yameandaliwa na Astan (Mfawidhi) wa kaburi takatifu la Imam Hussein (AS) katika mwezi wa Hijri wa Rajab (Janaury 23- Februari 21).

Taarifa zinasema maonyesho hayo yafanyika Bain-ul-Haramain, eneo lililo kati ya makaburi ya Haram Takatifu za  Imam Hussein (AS) na Hazrat Abbas (AS), kwa mnasaba wa Siku ya Qur'ani Duniani.

Katika maonyesho ya mwaka jana kulikuwa na kkazi mbalimbali zinazohusiana na Qur'ani Tukufu ikiwemo Misahafu tano ya kihistoriailiyoandikwa  kwa mkono, kazi za sanaa 63 za kihistoria zinazohusiana na Qur'ani Tukufu, na nakala 46 za Qur'ani Tukufu zilizochapishwa katika nchi mbalimbali.

Maonyesho hayo pia yalijumuisha kazi kutoka Syria, Iran, Misri, Indonesia, Jordan, Bahrain, Uturuki, Malaysia, Brunei, Libya, India, Pakistan, Saudi Arabia, Algeria, Morocco, Ujerumani, na Ufaransa.

Maonyesho hayo yalikuwa na vibanda tofauti, likiwemo la kufundishia wageni usomaji sahihi wa Qur'ani Tukufu.

Wakati huo huo, Sheikh Hassan al-Mansouri, mshauri wa Qur'ani wa Mfawidhi wa Haram Takatifu ya Imam Hussein AS, katika mkutano na Rafi al-Ameri, mkurugenzi wa Kituo cha Kitaifa cha Sayansi ya Qur'ani chenye mafungamano na Idara ya Waqf ya Mashia wa Iraq, alikialika kituo hicho kuhudhuria mwaliko ujao.

Pande hizo mbili pia zilijadili njia za kuimarisha ushirikiano katika nyanja za Qur'ani Tukufu na kuamsha harakati za Qur'ani Tukufu nchini Iraq.

Int’l Quran Exhibition Planned in Iraqi Holy City of Karbala

Int’l Quran Exhibition Planned in Iraqi Holy City of Karbala

4112359

captcha