Programu ya Qur'ani iliandaliwa na kituo cha Dar-ul-Quran chenye mfungamano na Idara ya Mfawidhi wa Haram au Kaburi Takatifu la Imam Hussein (AS).
Zaidi ya wanawake 80 kutoka Babil walichukua kozi, iliyoitwa Safinat-ul-Najat (Meli ya Wokovu).
Kozi hiyo ilijikita katika aya za Qur'ani Tukufu zinazofungamana na Imam Hussein (AS).
Afisa mkuu wa idara hiyo Sayed Murtadha Jamaledin na mratibu wa kozi za Qur'ani za idara hiyo kwa wanawake Umm Ilaf al-Halfi walikuwepo katika hafla ya kufunga kozi hiyo.
Hafal ilianza kwa usomaji wa aya za Qur'ani na Ali Musa na kisha Jamaledin akatoa hotuba kuhusu kozi maalumu za Qur'ani na kuhusu hadhi ya Imam Hussein (AS) kwa mujibu wa Qur'ani.
Huda al-Shammari, mkufunzi wa kozi hiyo, pia alitoa hotuba.
Kwingineko katika hafla hiyo washiriki waliopata nafasi za juu walipewa zawadi na vyeti vya mahudhurio vilikabidhiwa washiriki wote.
4250555