IQNA

Rais Ebrahim Raisi akiwa katika Haram ya Imam Khomeini (MA)

Mapinduzi ya Kiislamu yamezidi kudhihirika duniani licha ya fitna na njama zote za adui

18:41 - January 31, 2023
Habari ID: 3476494
TEHRAN (IQNA)- Rais Ebrahim Raisi amesema: Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran chini ya uongozi wa Imam Khomeini (MA) yamedumu licha ya fitna na njama zote za adui na yamezidi kudhihirika duniani.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyasema hayo leo katika hafla ya kutangaza tena baia na ahadi ya utiifu kwa malengo matukufu ya mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na akaongeza kuwa: Kwa ikhlasi na ukweli wa Imam Khomeini (MA) utiifu na mapenzi ya wananchi kwa Mapinduzi ya Kiislamu yameshamiri na baada ya kupita miaka 44 tangu ushindi wake, mapinduzi hayo yamejidhihirisha zaidi duniani licha ya fitna na njama zote za adui.
Rais Raisi amesema, kumekuwa na fitna nyingi za kuyaangamiza mapinduzi na urithi adhimu wa Imam Khomeini (MA) katika kipindi cha miongo minne iliyopita na akaongeza kuwa: Imam alikuwa na imani na wananchi na hii leo inapasa irada na matakwa ya wananchi yaendelee kutimizwa.
Seyyid Ebrahim Raisi ameashiria utiifu na mapenzi ya wananchi kwa Mapinduzi ya Kiislamu na akasema: "ishara ya mapenzi hayo ya wananchi ni mashahidi waliojitolea maisha yao kuyadumisha na kuyalinda mapinduzi."

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, njia ya kuwakinga vijana ni kuwaelewesha shakhsia ya muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu na sifa za Mapinduzi ya Kiislamu na akasema: wanautamaduni na waandishi inapasa wajue kwamba leo hii moja ya njia za kuikinga jamii na vijana ambao hawakumuona Imam Khomeini (MA) na vita ni kuhakikisha malengo matukufu ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yanabainishwa kwa jamii ya leo kwa kutumia sanaa.

Kwa mnasaba wa kuwadia maadhimisho ya Alfajiri Kumi za ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Rais Seyed Ebrahim Raisi na mawaziri wa serikali ya 13 ya Iran leo asubuhi walizuru haram ya Imam Khomeini (MA) na kutangaza tena baia na ahadi ya utiifu kwa malengo matukufu ya mwasisi huyo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Kesho Jumatano tarehe 12 Bahman 1401 Hijria Shamsia sawa na tarehe 1 Februari 2023, yanaanza maadhimisho ya Alfajiri Kumi za ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

4118701

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha