IQNA

Jinai za Israel

Hamas yasema Wapalestina watajibu jinai za utawala ghasibu wa Israel

21:36 - February 25, 2023
Habari ID: 3476625
TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imesisitiza kuwa, jinai za utawala ghasibu wa Israel zitajibiwa na wanamapambano shupavu wa Kipalestina na katu hazibakia hivi hivi bila ya majibu.

Taarifa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imetolewa kwa mnasaba wa kumbukumbu ya mauaji dhidi ya waumini katika msikiti wa Ibrahim huko al-Khalil Palestina.

Sehemu moja ya taarifa hiyo ya HAMAS imesisitiza kuwa, vita vya Wapalestina na utawala vamizi wa Israel ni vya daima na kwamba, Wapalestina wako imara na katu hawatasalimu amri.

Sehemu nyingine ya taarifa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imeyataka mataiifa na viongozii wa nchi za Kiislamu na Kiarabu kuliunga mkono taifa la Palestina kkatika mapambano na muqawama wake dhidi ya adui Mzayuni.

Itakumbukwa kkuwa, tarehe 25 Februari mwaka 1994 Mzayuni mmoja aliyekuwa na misimamo ya kufurutu ada aliwashambulia na kuwamiminia risasi Waislamu waliokuwa wakitekeleza ibada ya Swala katika Msikiti wa Haram ya Nabii Ibrahim mjini al Khalil, Palestina inayokaliwa kwa mabavu na kuua shahidi 29 miongoni mwao. Mauaji hayo yalitokea wakati Waislamu hao walipokuwa katika ibada ya funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Waislamu wengine wengi walijeruhiwa katika shambulizi hilo la kikatili. Mauaji hayo ambayo yalidhihirisha tena uhasama na chuki za Wazayuni wa Israel dhidi ya Waislamu, yalilaaniwa na Waislamu kote duniani. Ukatili huo ulizusha wimbi kubwa la machafuko katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina ambapo wananchi walizidisha mapambano dhidi ya maghasibu wa Tel Aviv. Israel ilimshika kwa muda na kumuachia huru mhalifu huyo katili kwa kisingizio kwamba alikuwa punguani.

4124287

captcha