IQNA

Mwezi wa Ramadhani

Mapendekezo Saba ya Kutoa Sadaka Mwezi wa Ramadhani

14:44 - March 28, 2023
Habari ID: 3476775
TEHRAN (IQNA) – Moja ya sababu za kufunga katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni kuelewa hali za watu masikini. Kwa hivyo, mojawapo ya mapendekezo makuu kwa wale wanaofunga mwezi huu mtukufu wa Ramadhani ni kutoa sadaka, hasa kwa wasio na uwezo.

Sadaka au sadaqa ni miongoni mwa mila za Kiislamu zilizosisitizwa sana wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Kulingana na kitabu cha "Kanz al-Maram fi Amal Shahr al-Siyam", mafundisho ya Kiislamu yanarejelea baadhi ya mambo muhimu kuhusu sadaka ifuatavyo.

1) Kutoa sadaka ambayo imtokana na chumo la Halali: "Enyi mlio amini! Toeni katika vile vizuri mlivyo vichuma, na katika vile tulivyo kutoleeni katika ardhi. " (Surah Al-Baqarah, aya ya 267)

2) Kulinda hadhi na heshima ya maskini wanaopokea sadaka: Mtume Muhammad (SAW) amesema: “Kutoa sadaka kwa siri huizima ghadhabu ya Mwenyezi Mungu.”

3) Kutoa anachokipenda mtu: "Hamtapata wema mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda. Na kitu chochote mnacho kitoa basi hakika Mwenyezi Mungu anakijua.” (Surah Al-Imran, aya ya 92)

4) Kutoa Sadaka kabla ya mwenye haja kuuliza: Kwa mujibu wa Hadithi na riwaya ni bora kuwasaidia masikini kabla hajaomba msaada.

5) Sadaka bila lawama: "Enyi mlio amini! Msiharibu sadaka zenu kwa masimbulizi na maudhi, kama anaye toa mali yake kwa kuwaonyesha watu, wala hamuamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho." (Surah Al-Baqarah, aya, 264)

6) Kuwasaidia jamaa wahitaji, Mtume Muhammad (SAW) amesema: “Sadaka iliyo bora zaidi ni ile inayotolewa mtu akiwa tajiri, na mkono wa kutoa ni bora kuliko kuchukua, na unapaswa kuanza kwanza kuwasaidia wanaokutegemea (jamaa).

Katika hadithi nyingine, Mtukufu Mtume (SAW) anasema si sawa kutoa sadaka kwa wengine wakati  jamaa wa karibu wa mtu wanahitaji msaada.

7) Kuzingatia wakati na mahali: Wakati na mahali pa kutoa sadaka huathiri malipo. Kwa hiyo, Waislamu wanapendekezwa kuwasaidia maskini na kutatua matatizo ya watu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

3482960

captcha