IQNA

Mwezi wa Ramadhani

Milo 8.5 ya Iftar kusambazwa miongoni mwa waumini katika Msikiti wa Mtume SAW Mwezi wa Ramadhani

21:03 - February 11, 2024
Habari ID: 3478338
IQNA - Zaidi ya milo ya Iftar (futari) milioni 8.5 itagawiwa kwa waumini katika Msikiti wa Mtume SAW, Al Masjid An Nabawi huko Madina wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Al Masjid An Nabawi, eneo la pili kwa Uislamu katika mji wa Madina, limeandaliwa vyema kuwapokea waumini wanaotarajiwa kumiminika kwa wingi mahali hapo wakati wa Mwezi wa Ramadhani.

Zaidi ya milo ya Iftar milioni 8.5 inatarajiwa kugawiwa kwa waumini msikitini wakati wa Ramadhani, unaotarajiwa kuanza mwaka huu Machi 11.

Aidha chupa milioni 2.5 za maji ya Zamzam pia zitatolewa kwenye Al Masjid An Nabawi wakati wa mwezi wa Ramadhani

Aidha, msikiti huo utawekewa kontena 18,000 za maji ya Zamzam.

Katika kuelekea Ramadhani, Mamlaka Kuu ya Utunzaji wa Al Masjid An Nabawi ilifanya warsha kuhusu maandalizi ya mwezi huo mtukufu.

Katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani idadi kubwa ya Waislamu pia hutekeleza ibada ya Hija ndogo ya Umrah au hija ndogo katika Msikiti Mkuu wa Makka, Masjid al Haram, eneo takatifu zaidi katika Uislamu, huko Makka na baada ya hapo huelekea Al Masjid An Nabawi­­­­­­ kuswali katika msikiti huo na kutembelea maeneo mengine ya Kiislamu mjini humo.

Zaidi ya Waislamu milioni 280 walisali katika Msikiti wa Mtume mwaka jana, kulingana na takwimu rasmi. Msikitini hapo kuna  Al Rawda Al Sharifa, eneo lilipo kaburi la Mtume Muhammad (SAW).

3487143

Habari zinazohusiana
captcha