IQNA

Hali ya Waislamu

Wanafunzi Waislamu waendelea kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu huko Korea Kusini

16:57 - April 27, 2023
Habari ID: 3476923
TEHRAN (IQNA) – Kundi la wanafunzi Waislamu wanaendelea kupigania haki yao ya kuwa na mahali pa ibada huko Daegu, Korea Kusini, huku kukiwa na unyanyasaji wa chuki dhidi ya Uislamu katika eneo hilo.

Huko Daegu, Korea Kusini, wanafunzi Waislamu wamekuwa wakitumia nyumba kusali kwa miaka mingi. Sasa wanajenga msikiti, na katika mchakato huo, wanapambana na chuki dhidi ya Uislamu katika eneo hilo.

Ujenzi wa msikiti huo ulianza mnamo 2020, lakini umesitishwa mara kadhaa kutokana  uingiliaji wa serikali za mitaa, vizuizi mbali mbali huku polisi wakikataa kuchukua hatua kukabiliana na wale wanaowasumbua Waislamu.

Licha ya ujenzi wa msikiti kupata idhini ya kisheria, unyanyasaji kutoka kwa vikundi vya chuki dhidi ya Uislamu unaendelea, ikiwa ni pamoja na kuweka vichwa vya nguruwe nje ya lango la msikiti.

Wakati majirani wengi walikuwa wamekubali ujenzi wa msikiti hapo awali, wanaopinga msikiti huo wanaendelea kupata nguvu, kwa kuungwa mkono na vikundi mbali mbali

Waumini katika  misikiti huo hivi karibuni waliwasilisha kesi yao kwa vyombo vya habari vya kigeni, wakielezea kutokuwepo kwa uungaji mkono wa serikali ya Korea Kusini kwa haki za binadamu.

Nje ya msikiti, karamu ya nyama choma ya nguruwe ambayo hufanywa mara kwa mara ni ishara ya kina cha chuki dhidi ya Uislamu, huku makundi yanayopinga Uislamu yakipanga mikutano mikubwa. Waislamu wa eneo hilo wakizungumza na televisheni ya Press TV wanasema kampeni dhidi ya msikiti huo inaongozwa na kundi moja la makasisi Wakristo ambao wanafanya juu chini kuhakikisha kuwa ujenzi wa msikiti huo unasitishwa.

3483341

Kishikizo: waislamu korea kusini
captcha