IQNA

Waislamu Ujerumani

Msikiti wa Ujerumani wapokea barua yenye vitisho na matusi

17:05 - December 14, 2023
Habari ID: 3478036
IQNA - Barua ya vitisho imetumwa kwa msikiti katika mji wa Magharibi mwa Ujerumani wa Munster.

Barua hiyo inayoashiria hisia za chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu ilitumwa kwenye Msikiti wa Munster Central, ambao unafungamana  na Kundi la Waturuki-Waislamu Ujerumani DITIB, ilikuwa na matusi dhidi ya Waislamu na wahamiaji, afisa wa kidini alisema Jumatano.
Pia ilikuwa na matamshi ya kibaguzi, yakiwemo "Ujerumani kwa Wajerumani, wageni nje."
Akizungumza na Shirika la Habari la Anadolu, Fettah Cavus, mkuu wa Jumuiya ya Msikiti Mkuu wa Munster, alisema kuwa kwa masikitiko, chuki dhidi ya wageni na Waislamu inaongezeka nchini Ujerumani.
Alisema wakiwa jumuiya ya Kiislamu, wanadai mhusika au wahusika wakamatwe na wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.

 

Kishikizo: ujeurmani waislamu
captcha