Akizungumza katika kipindi katika Redio ya Goftogo ya Iran, Jalil Bayt Mashaali, ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA), alitaja "ikhlasi na ukweli", "uthabiti na kuwa sawasawa maneno", "uadilifu", “hekima” na “kuwasilisha ujumbe kutoka kwa mtazamo wa Rifq” kuwa misini hiyo mitano kanuni tano.
Amesema uaminifu na ukweli ni kigezo cha kwanza muhimu katika kutoa ujumbe.
Wakati ukweli unafungua mioyo, "ujinga wa kisasa", ambao umeondoka kwenye Fitra ya binadamu (asili), unawataka waandishi habari kusema uwongo mkubwa, alisema.
Ameongeza kuwa Qur'ani Tukufu pia imesisitiza ulazima wa kufanya mambo kwa njia iliyo bora zaidi na ndiyo maana katika kufikisha ujumbe ni muhimu kutumia kauli zenye sauti sawa na Qur'an Tukufu inavyosema: “Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu na semeni maneno ya sawasawa." (Aya ya 70 ya Surah Al-Ahzab)
Afisa huyo alisema neno Sadeed katika aya hii maana yake ni thabiti na sahihi na ikiwa kauli ni thabiti na sahihi, matokeo yatakuwa, “Apate kukutengenezeeni vitendo vyenu na akusameheni madhambi yenu..” (Aya ya 71 ya Surat Al-Ahzab)
Kisha Bayt Mashaali amesisitiza nafasi ya uadilifu katika upashanaji wa ujumbe na akasema Qur'ani Tukufu inaiwekea umuhimu.
Amesema uadilifu ndio msingi wa kufaulu katika njia ya Taqwa (kumcha Mungu) na huitengenezea njia, kama Qur'ani inavyosema, “Enyi mlio amini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mkitoa ushahidi kwa haki. Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mno na uchamngu. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.” (Aya ya 8 ya Surah Al-Ma’idah)
Mkurugenzi mkuu wa IQNA pia ameashiria kanuni ya hekima na kusema kuwasilisha ujumbe na vyombo vya habari kunapaswa kufanywa kwa busara ili kuwa na ufanisi na kutatua matatizo ya jamii.
3490713