IQNA

Watetezi wa Qur'ani Tukufu

Baada ya mashinikizo, Denmark yaamua kupiga marufuku vitendo vya kuvunjia heshima Qur'an Tukufu

15:47 - August 25, 2023
Habari ID: 3477492
TEHRAN (IQNA)- Mahakama ya Denmark imeamua kupiga marufuku kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu kufuatia taathira mbaya za hatua hizo.

Waziri wa Sheria wa Denmark aliwaambia waandishi wa habari siku ya Ijumaa kwamba serikali itawasilisha mswada ambao "utapiga marufuku kuvunjia heshima kila ambacho kina umuhimu mkubwa wa kidini kwa jamii ya kidini."

Waziri wa Sheria Peter Hummelgaard alisema sheria hiyo inalenga hasa uvunjiaji heshima unaofanywa na watu wachache katika maeneo ya umma katika taifa la hilo Skandinavia jambo ambalo limewakasirisha Waislamu duniani.

Katika kitendo cha hivi punde zaidi cha kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu katika nchi jirani ya Uswidi, mtu mmoja ambaye ametenda vitendo vya kuvunjia heshima Kitabu Kitukufu cha Waislamu alikichoma moto mbele ya ubalozi wa Iran mjini Stockholm.

Badala ya kuzuia kitendo hicho, polisi wa Uswidi badala yake walimkamata mwanamke aliyejaribu kumzuia mhalifu huyo.

Hatua hizo za kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu, ambazo zimeidhinishwa na polisi wa Uswidi kwa kisingizio cha sheria za uhuru wa kujieleza, zimeibua hasira ya ulimwengu wote wa Kiislamu, na kusababisha kufukuzwa wanadiplomasia Uswidi na Denmark kutoka nchi kadhaa.

Mapema mwezi huu, akizungumza katika mazungumzo ya simu na mwenzake wa Denmark, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amir-Abdollahian alieleza kuwa, kuvunjiwa heshima kwa Qur'ani Tukufu kunaumiza hisia za Waislamu wote katika nchi za Kiislamu na hivyo basi lazima serikali ya nchi hiyo ichukua hatua kusitisha vitendo hivyo viovu.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Denmark Lars Lokke Rasmussen kwa upande wake alieleza masikitiko yake makubwa kutokana na vitendo hivyo na kusisitiza kuwa serikali ya nchi yake inalaani vikali kitendo chochote cha kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu.

Mwanadiplomasia wa Denmark alisema uhuru wa kujieleza unaruhusiwa na sheria ya Denmark, lakini alionyesha masikitiko kwamba baadhi ya watu wanautumia vibaya, "jambo ambalo tunaliona kuwa halikubaliki." "Watu hawa wachache hawapaswi kuchukuliwa kuwa wawakilishi wa watu wa Denmark."

4164854

Habari zinazohusiana
captcha