IQNA

Zaidi ya wafanyaziyara Milioni 22 walitembelea mji Mtukufu Wa Karbara Msimu Wa Arubaini

11:03 - September 09, 2023
Habari ID: 3477570
KARBALA (IQNA) - Zaidi ya wafanyaziyara milioni 22 walitembelea mji Mtukufu wa Karbala katika msimu wa mwaka huu wa Arubaini hadi sasa.

Hii ni kwa mujibu wa Astan (ulezi) wa kaburi tukufu  la Hazrat Abbas (AS) ambalo lilisema idadi ya wafanyaziyara wa Arubaini ilizidi milioni 22.02 kufikia Jumatano alasiri.

Wakati huo huo, Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Iraq (ICAA) ilisema kuanzia mwezi  Agosti tarehe  15 hadi mwezi  Septemba tarehe  3, jumla ya safari za ndege 1,850 zilileta Wafanyaziyara 250,000 kutoka nchi mbalimbali hadi Iraq kwa Arubaini.

Wafanyaziyara wengi zaidi wa kigeni waliwasili katika nchi hiyo ya Kiarabu kupitia vivuko vya mpaka wa nchi kavu.

Katika habari nyingine zinazohusiana, Khalid al-Muhanna, msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Iraq, alisema mpango maalum wa usalama wa Arubaini, umetekelezwa kwa mafanikio hadi sasa na utaendelea hadi kurejea nyumbani kwa hujaji wa mwisho.

Sherehe ya maombolezo ya Arubaini inasimama kama kutaniko la kidini la ajabu na kubwa katika kiwango cha kimataifa.

Waja wa Imam Hussein (as)  Wafanya Ibada za Maombolezo huko Karbala huko Arbaeen

Tukio hili kubwa linaashiria siku ya 40 baada ya Ashura, ukumbusho adhimu wa kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), mjukuu  wa Mtume Muhammad (SAW).

Kila mwaka umati mkubwa wa Mashia humiminika Karbala, ilipo Haram tukufu ya Imam Hussein (AS) kufanya ibada za maombolezo.

Wafanyaziyara, hasa kutoka Iraq na Iran, husafiri njia ndefu kwa miguu hadi mji mtukufu wa Karbala.

 

3485075

 

 

Kishikizo: mahujaji karbala milioni
captcha