Iliandaliwa na Kituo cha Vyombo vya Habari vya Qur'ani cha Dar-ol-Quran kinachofungamana na Idara ya Mfawidhi wa Haram ya Imam Hussein (AS).
Kozi hii ilijumuisha maeneo matatu kuu: uandishi wa habari, upigaji picha, na uarifishaji wa miduara ya Qur'ani.
Kulikuwa na washiriki kutoka matawi ya Kituo cha Dar-ol-Quran katika majimbo 15 ya Iraq.
Kwa mujibu wa Wassam Nadhir al-Dalfi, mkuu wa Kituo cha Vyombo vya Habari vya Qur'ani, ilikuwa ni kozi ya pili iliyolenga kukuza taasisi za habari zilizo na uhusiano na matawi ya kituo hicho kote Iraq, na ililenga kuboresha ujuzi wa wafanyakazi wa vyombo vya habari.
Tukio hilo lilianza na kisomo cha Ali Mousa, msomaji na mwanaharakati wa vyombo vya habari, kikifuatiwa na hotuba kutoka kwa Sheikh Khair al-Din Hadi, mkuu wa Dar al-Quran.
Katika hotuba yake, Sheikh Hadi alisema kuwa jitihada za vyombo vya habari, kama misheni, zinapaswa kuwasilishwa kwa njia bora zaidi kwa kuzingatia ubunifu na uvumbuzi.
Alisema kuwa Qur'ani ina ujumbe muhimu kwa yombo vya habari kwa ajili ya kuongoza jamii.
Alisisitiza pia umuhimu wa misheni ya vyombo vya habari katika hali ya sasa, na umuhimu wa kusaidia vyombo vya habari vya Qur'ani na kuwasilisha ujumbe wa Qur'ani kwa jamii.
3491371