IQNA

Harakati za Qur'ani

Kituo cha Karbala Dar-ul-Quran kimeandaa kozi tatu za Qur’ani mtandaoni

20:40 - December 15, 2024
Habari ID: 3479900
IQNA - Kozi tatu za kimataifa za mtandaoni zinazojumuisha masomo ya Qur’ani Tukufu zimeandaliwa huko Karbala, Iraq.

 

Kituo cha Dar-ul-Quran chenye mfungamano na Idara ya Mfawidhi wa  haram takatifu ya Imam Hussein (AS), kimeandaa kozi hizo kwa kushirikisha wanafunzi wa Qur'ani kutoka nchi mbalimbali.

“Kampeni ya Qur’ani; Aya kuhusu Imam Hussein (AS)”, “Nur al-Quran; Aya kuhusu Imam Mahdi (AS)”, na “Funguo za Kwanza na za Mwisho za Sayansi; Sunnah za Qurani” ni mada za kozi hizo za Qur'ani.

Sayyed Murtadha Jamaleddin, naibu wa kitaaluma wa kituo hicho, anasimamia kozi za mtandaoni.

Amebaini kuwa masomo yanatolewa kupitia maonyesho ya video na sauti na faili za PDF.

Alisema zana za hivi punde za mtandao zimetumika kuwasaidia wanafunzi.

Jamaleddin ameongeza kuwa, kozi hizo zinalenga kukuza utamaduni na maadili ya Qur'ani miongoni mwa kizazi cha vijana.

Vile vile vinakusudiwa kuimarisha mafungamano ya wanafunzi na Kitabu kitukufu kupitia aya kuhusu Sirah ya Ahl-ul-Bayt (AS), alisema.

Kituo cha Dar-ul-Quran kimekuwa kikitengeneza programu za kufundisha Qur'ani kwa kutumia teknolojia za kisasa kabisa.

3491044

Habari zinazohusiana
Kishikizo: qurani tukufu karbala
captcha