IQNA

Mwanamume Aliyepatikana na Hatia ya Kuchochea Chuki za Kikabila kwa Kuchoma Qur’ani Tukufu nchini Swedeni

13:25 - October 14, 2023
Habari ID: 3477728
STOCKHOLM (IQNA) – Mwanamume aliyepatikana na hatia ya kudhalilisha nakala ya Qu’rani Tukufu nchini Swedeni na kuweka video hiyo mitandaoni amewekwa hatiani kwa kuchochea chuki za kikabila dhidi ya Waislamu.

Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 27 alijipiga picha nje ya kanisa kuu la Linkoping mwezi Septemba  mwaka 2020, akichoma Qur'ani Tukufu na nyama  ya  ng'ombe yenye ishara ya dharau kuhusu Mtume Muhammad (SAW), Kisha alishiriki video hiyo kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii ya X na YouTube, na kuacha Qur’ani Tukufu na nyama iliyoteketezwa nje ya msikiti wa Linkoping.

Mahakama ilisema kitendo chake kililenga Waislamu na sio Uislamu kama dini, na kwamba hakikuchangia mjadala wowote wa kujenga.  

Video hiyo pia ilikuwa na wimbo uitwao Ondoa Kababu, ambao ni maarufu miongoni mwa vikundi vya mrengo mkali wa kulia na unatoa wito wa kufukuzwa kwa Waislamu,Mahakama ilisema wimbo huo unahusishwa pakubwa na mauaji ya Christchurch ya 2019, ambapo kiongozi wa kizungu aliwaua watu 51 katika misikiti miwili huko New Zealand.  

Mwanaume akabiliwa Na Kesi Kwa Kuchochea Chuki Dhidi Ya Waislamu Kwa Kuchoma Qur’ani Tukufu.

Mwanamume huyo alidai kuwa alikuwa akiukosoa Uislamu kama dini, lakini mahakama ilikataa hoja yake, Mahakama ilisema hatua yake hiyo ni dhahiri ililenga kuonyesha vitisho na dharau kwa Waislamu, na kwamba haiwezi kutafsiriwa kwa njia nyingine yoyote.  

Mwanamume huyo alipatikana na hatia ya machafuko dhidi ya kikundi cha kikabila, ambayo ni mara ya kwanza kwa mfumo wa mahakama ya Swedeni kujaribu shitaka hili la kudhalilisha Qu’rani Tukufu.  

Mahakama iliona kuwa muziki uliochaguliwa kwenye filamu yenye maudhui kama haya hauwezi kutafsiriwa kwa njia nyingine yoyote isipokuwa kuwa tishio dhidi ya Waislamu kwa kuashiria imani yao, mahakama iliandika katika taarifa yake na kuongeza, Maudhui ya filamu na namna ya uchapishaji wake ni kwamba ni wazi kwamba lengo kuu la mshtakiwa lisingeweza kuwa zaidi ya kutoa vitisho na dharau, Mahakama bado haijatangaza hukumu ya mtu huyo.

 


3485554

 

captcha