IQNA

Diplomasia ya Utamaduni

Mjumbe wa Utamaduni aangazia mazungumzo baina ya dini kati ya Iran, Uhispania

15:34 - December 09, 2023
Habari ID: 3478011
MADRID (IQNA – Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Uhispania amesisitiza haja ya maendeleo ya mazungumzo baina ya dini mbali mbali katika nchi hizi mbili.

Akizungumza katika mahojiano na IQNA, Mohammad Mehdi Ahmadi alisema mashirika ya Kikristo nchini Uhispania yana nia na yanaamini katika mazungumzo. "Sisi nchini Iran pia tunaamini katika mazungumzo na tunayaona kuwa ya manufaa," alisema.

Kumekuwa na midahalo kuhusu masuala kama vile amani, haki ya kijamii na masuala ya kidini na midahalo kama hiyo itaendelea katika siku zijazo, alisema.

Ahmadi aliongeza kuwa wajumbe wa wanazuoni na viongozi wa kidini wanapaswa kufanya ziara za maelewano ili kupanua mazungumzo.

Vile vile amebainisha kuwa, Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Uhispania kinapanga kuandaa kongamano kuhusu misingi ya kidini kwa mitazamo ya Uislamu na Ukristo.

Kongamano hilo linatazamiwa kufanyika mwezi Februari-Machi 2024, kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Salamanca, ambacho kinaendeshwa chini ya usimamizi wa Kanisa Katoliki, alisema.

Kwingineko katika mahojiano hayo, Ahmadi aligusia hali ya Waislamu nchini Uhispania, akisema kuna Waislamu wapatao milioni 2.2 nchini humo, ambayo ina wakazi milioni 47.

Asilimia kumi ya Waislamu wa nchi hiyo ni Wahispania asili na waliosalia wanatoka katika nchi nyinginezo, kama vile Morocco, Jordan, na Iraq.

Alisema karibu asilimia tano ya Waislamu wa Uhispania wanafuata madhehebu ya Shia na waliosalia ni wa madhehebu ya Sunni.

Taasisi za Kiislamu zimeunda umoja na kuandaa programu za Kiislamu, na serikali ya Uhispania inaziunga mkono, alibainisha.

Kuhusu Islamophobia, mjumbe wa Iran alisema vyama vinavyopinga Uislamu havifanyi kazi nchini Uhispania kama vile vya nchi kama Uholanzi na Denmark.

3486343

Pia aliangazia uungwaji mkono kwa Palestina miongoni mwa vyama vya kisiasa nchini Uhispania.

Kishikizo: uhispania iran waislamu
captcha