IQNA

Mwanaharakati wa Kuwait

Vita dhidi ya Gaza vimewafedhehesha wanaodai kutetea haki zabinadamu

22:40 - January 20, 2024
Habari ID: 3478223
IQNA - Mwanaharakati mmoja wa Kuwait alielezea hali ya sasa ya Palestina na vita vya mauaji ya halaiki vinavyoendeshwa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ghaza kuwa ni fedheha kwa nchi zinazodai kuwa watetezi wa haki za binadamu.

Hassan al-Qarashi, ambaye ni mwanachama wa mashirika ya kutetea haki za binadamu ya nchi hiyo ya Kiarabu, aliiambia IQNA katika mahojiano kwamba uungaji mkono wa serikali za Magharibi kwa ukatili wa utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza ulionyesha unafiki wao linapokuja suala la kutetea haki za binadamu.

Amesema pamoja na madai yao yote hayo, nchi za Magharibi ni washirika katika jinai za Israel, ikiwemo mauaji ya wanawake na watoto wa Kipalestina na kuzingirwa kikamilifu Gaza.

Al-Qarashi alisifu uungwaji mkono kwa watu waliodhulumiwa wa Palestina miongoni mwa mataifa mbali mbali ya dunia.

Tangu ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya 1979, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia imeweka uungaji mkono wa Palestina juu ya ajenda yake na imeligeuza suala la Palestina kuwa suala nambari moja la ulimwengu wa Kiislamu, ameongeza.

Leo, watu wa dunia wameungana katika kuunga mkono watu wa Palestina na sababu, alisisitiza.

Kwingineko katika matamshi yake, mwanaharakati huyo wa Kuwait alikashifu hatua ya baadhi ya nchi za Kiarabu ya kurejesha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni, akisema hatua hiyo haina matokeo chanya ama kwa kutatua suala la Palestina au kwa watu wa mataifa hayo ya Kiarabu.

Serikali za nchi hizi lazima ziheshimu matakwa ya watu wao na kuacha kuhalalisha uhusiano na utawala wa Israel, aliongeza.

IQNA ilimhoji al-Qarashi kando ya kongamano la kimataifa lililopewa jina la ‘Dhoruba ya Al-Aqsa na Mwamko wa Dhamiri ya Binadamu’ uliofanyika mjini Tehran Jumapili iliyopita.

Zaidi ya shakhsia 100 wa Kiislamu duniani, wanazuoni na wanafikra waliohudhuria mkutano huo walifafanua kuhusu Jihadi ya watu wa Ukanda wa Gaza na matokeo ya Operesheni ya Mafuriko ya Al-Aqsa, ambayo harakati ya muqawama ya Hamas ya Palestina ilianzisha dhidi ya utawala wa Kizayuni tarehe 7 Oktoba, 2023.

3486873

captcha