IQNA

Wapalestina 100,000 wameswali katika Msikiti wa Al-Aqsa Siku ya 25 ya Ramadhani

16:49 - March 26, 2025
Habari ID: 3480443
IQNA – Wapalestina wanaendelea kushiriki katika Swala za jamaa katika Msikiti wa Al-Aqsa katika jiji takatifu la al-Quds kwa wingi wakati wa Ramadhani licha ya vizuizi vinavyowekwa na utawala dhalimu wa Israel.

Takriban Wapalestina 100,000 walishiriki katika Swala ya Taraweeh siku ya 25 ya mwezi mtakatifu wa Ramadhani katika msikiti huo siku ya Jumanne.

Taarifa ya Idara ya Wakfu ya al-Quds na Idara ya Mambo ya Msikiti wa Al-Aqsa, ambayo inawajibika kwa usimamizi wa eneo hilo, imebaini kwamba wengi wa waumini hao 100,000 walikuwa wakaazi wa al-Quds. Hata hivyo, maelfu ya Wapalestina kutoka maeneo mbali mbali katika Ukingo wa Magharibi, unaokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu Israel, walizuiwa kuingia al-Quds kutokana na vituo vya ukaguzi vya kijeshi vya utawala huo.  

Vizingiti hivyo vimewekwa na Israel tangu mwanzo wa Mwezi Mtukufu Ramadhani ambapo vijana wanazuiwa kushiriki katika Swala msikitini hapo. Msikiti wa Al-Aqsa, moja ya maeneo matakatifu zaidi katika Uislamu, kwa kawaida hushuhudia idadi kubwa ya Wapalestina wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Kwa hofu ya mkusanyiko mkubwa wa Waislamu, vikosi vya utawala wa Kizayuni wa Israel mara nyingi huweka vikwazo vya kufika katika msikiti huo.

3492503

Kishikizo: al aqsa ramadhani swala
captcha