Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB, helikopta iliyombeba Seyed Ebrahim Raisi, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na ujumbe aliofuatana nao-, ambao jana Jumapili walielekea Azerbaijan Mashariki kukagua Bwawa la Khoda Afarin na kuzindua miradi kadhaa ya kitaifa na ya mkoa-, ilipata ajali na kuanguka wakati ikitoka kwenye eneo la bwawa hilo kuelekea Kiwanda cha Usafishaji Mafuta cha Tabriz kutokana na hali mbaya ya hewa iliyokuwepo katika eneo la Varzghan.
Licha ya kutumwa vikosi kadhaa vya uokoaji vya usaidizi wa haraka ili kutoa huduma kwa Rais na walioandamana nao, juhudi za kuipata helikopta iliyoanguka zilichukua masaa mengi kutokana na hali ya hewa ya ukungu na ugumu wa kupita kwenye eneo la misitu na milima.
Kufuatia ajali hiyo, Baraza la Mawaziri limefanya kikao cha dharura.
3488410