IQNA

Maombolezo

Makundi ya Muqawama yaomboleza kufa shahidi Rais Raisi wa Iran

23:42 - May 20, 2024
Habari ID: 3478857
IQNA-Makundi ya mapambano ya Kiislamu (muqawama) katika eneo la Asia Magharibi yametuma salamu za rambirambi na kuonyesha mshikamano na taifa na serikali ya Iran kufuatia ajali ya helikopta jana ambayo helikopta ambayo ilipelekea kufa shahidi Seyyed Ebrahim Raisi, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Amir Abdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje na wote waliokuwa katika msafaraha huo.

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, imetuma salamu zake za rambirambi kufuatia tukio hilo.

Hamas imebainisha "hisia za huzuni na uchungu pamoja na ndugu zao wa Iran na kutangaza mshikamano kamili na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika tukio hilo la kusikitisha."

Taarifa hiyo imesema mashahidi hao, "walikuwa na misimamo ya heshima ya kuunga mkono kadhia ya ukombozi wa Palestina" na "mapambano halali ya taifa la Palestina dhidi ya utawala wa Kizayuni."

Hali kadhalika Hamas imesema: "Walifanya juhudi za dhati na kuonyesha mshikamano na eneo thabiti la Ukanda wa Gaza" na pia walijitahidi kukabiliana na uchokozi wa Wazayuni dhidi ya watu wetu wa Palestina."

Hamas imebaini kuwa: "Tuna imani kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaweza, kwa irada ya Mwenyezi Mungu, kuondokana na athari za hasara hii kubwa, kwani wananchi wapenzi wa Iran wanazo taasisi zilizojiimarisha zenye uwezo wa kukabiliana na msiba huu mkubwa"

Nayo Kamati ya Muqawama Palestina imetoa taarifa ya rambirambi na kusema: 

"Palestina, watu wake, na wanamuqawama kamwe hawatasahau michango iliyotolewa na mashahidi wawili wa muqawam, Rais Ebrahim Raisi na Waziri wa Mambo ya Nje Dk. Hossein Amir-Abdollahian, katika kuunga mkono kadhia ya Palestina na utetezi kwa watu wetu katika majukwaa yote. Tuna imani kamili kuwa taifa adhimu la Iran na uongozi wao wenye busara wataibuka washindi katika mtihani huu mgumu, kama vile Iran imekuwa ikishinda nyakati zote zenye changamoto iliyokabili. Iran daima itasalia kuwa muungaji mkono imara wa watu wote wanaodhulumiwa wa Palestina na dunia katika kukabiliana na madola ya kibeberu na kidhalimu  duniani kote."

Nayo harakati ya Jihad Islami ya Palestina imetoa taarifa na kusema: "Kuuawa shahidi Rais na Waziri wake wa Mashauri ya Kigeni kunawakilisha hasara kubwa kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutokana na uwepo wao muhimu na mashuhuri katika safari ya Iran ya kuendelea kuwepo katika jukwaa la kisiasa la kimataifa na kieneo. Kufariki kwa wawili hao pia ni hasara kubwa kwa wananchi wa Palestina katika zama hizi ngumu, kwani walikuwa na nafasi kubwa na ya wazi katika kuunga mkono mkono mapambano na muqawama wa wananchi wa Palestina, na katika kukabiliana na uvamizi wa jinai unaoendelea wa Wazayuni. Tuna hakika kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina uwezo wa kukabiliana na msiba huu mkubwa kwani imeshinda matatizo na changamoto zote katika historia yake ya miongo mingi. Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu azipokee roho hizi zilizobarikiwa, azifunike katika rehema yake kubwa, na aziweke peponi."

Kwa upande wake, Harakati ya Kidemokrasia ya Ukombozi wa Palestina imetuma salamu za rambirambi kwa taifa la Iran na kubaini kuwa: "Kufa shahidi kwa Rais wa Iran Ebrahim Raisi, Waziri wa Mambo ya Nje Dkt. Hossein Amir-Abdollahian, na ujumbe waliofuatana nao katika ajali ya helikopta kumeleta mshtuko mkubwa katika Harakati ya Kidemokrasia ya Ukombozi wa Palestina, watu wetu na watu wapenda uhuru wa Palestina na dunia. Hii ni kutokana na nafasi kubwa inayotekelezwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika ngazi ya kieneo na kimataifa. Watu wetu, walimfahamu Marehemu Rais shahidi Ebrahim Raisi, na Marehemu Waziri, Shahidi Dk. Hossein Amir-Abdollahian, chini ya uongozi wa Mtukufu na Kiongozi wa Mapinduzi, Imam Ali Khamenei, kuwa ni wakweli, wapiganaji wanaotetea maslahi ya nchi yao na kukabiliana na njama dhidi yake. Zaidi ya hayo, mashahidi hawa wawili  walichukua jukumu kubwa katika kuwatumikia watu wetu, kazi yetu na haki zetu halali za kitaifa."

Huko Yemen, Mohammed Ali al-Houthi, Mkuu wa Kamati Kuu ya Mapinduzi, ametuma "rambirambi" zake kwa watu wa Iran na familia za maafisa waliokufa shahidi katika ajali hiyo.

Mohammed Abdulsalam, Msemaji wa Ansarullah ya Yemen, naye amesema kwamba kufariki dunia Rais Raisi "sio tu hasara kwa Iran bali pia ni hasara kwa ulimwengu wa Kiislamu, hasa kwa Palestina na Gaza."

Harakati ya muqawama ya Hizbullah ya Lebanon pia imemtaja rais wa Iran kama "ndugu na muungaji mkono mkubwa' wa harakati hiyo ya mapambano ya Kiislamu (muqawama) ya Lebanon. Taarifa hiyo imesema: "

Tumemfahamu Mwadhama Rais aliyeuawa shahidi kwa muda mrefu; alikuwa ndugu yetu mkubwa, muungaji mkono thabiti, na mtetezi shupavu wa mambo yetu na sababu za taifa, aliyetangulia miongoni mwao Al-Quds na Palestina, na mlinzi wa harakati za muqawama na wapiganaji wao katika misimamo yote ya jukumu alilokuwa nalo. Alikuwa mtumishi mwaminifu na mwaminifu wa wananchi wapendwa wa Iran na mfumo wa fahari wa Jamhuri ya Kiislamu, na muungaji mkono mwaminifu wa Mtukufu Imam Kiongozi, kivuli chake kidumu, na alikuwa tumaini kubwa kwa wote waliodhulumiwa.. Vile vile, ndugu mpendwa shahidi Dk. Huossein Amir-Abdollahian, katika nyadhifa zake zote za uwajibikaji, ambapo wa mwisho alikuwa katika Wizara ya Mambo ya Nje, alikuwa waziri mchapakazi na mwenye kujitolea,  akibeba bendera katika nyanja zote za kisiasa na kidiplomasia, vikao vya kimataifa na mpenda harakati za muqawama ."

3488414/

Habari zinazohusiana
captcha