IQNA

Maombolezo

Taifa la Iran katika majonzi wakati huu wa siku 3 za kuuaga mwili wa Shahidi Raisi na wenzake

16:31 - May 21, 2024
Habari ID: 3478859
IQNA - Idadi kubwa ya Wairani huko Tabriz wameshiriki katika shughuli ya kumuaga shahidi Rais Ebrahim Raisi na maafisa kadhaa waliokufa shahidi pamoja naye katika ajali mbaya ya helikopta iliyotokea Mei 19 milimani katika mkoa wa Azarbaijan Mashariki, kaskazini-magharibi mwa Iran.

Marasimu ya kuwaaga mashahidi hao wa ajali ya helikopta ya juzi yalianza leo asubuhi katika mji wa Tabriz na kuvuta umati mkubwa wa watu. Waombolezaji waliandamana kando ya majeneza ya mashahidi huku yakiwa yamepambwa kwa bendera ya taifa ya Iran.

Waombolezaji walikuwa wakipiga nara wakiahidi kumtii Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei na misingi ya Mapinduzi ya Kiislamu. Wameahidi pia kusimama imara dhidi ya adui wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. 

Akizungumza  katika shughuli hiyo ya kuwaaga na kutoa heshima za mwisho huko Tabriz, Ahmad Vahidi Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran amesema kuwa Iran inaomboleza msiba wa kumpoteza Rais mpenda, mashuhuri na mnyenyekevu."  Amesema Iran pia imehuzunishwa na kifo cha Hossein Amir Abdollahian Waziri wa Mambo ya Nje aliyeacha diplomasia hai katika nyakati nyeti za mapambano kama urithi wake.   

Kesho Jumatano Kiongozi Muadhamu ataongoza Sala ya maiti ya mashahidi hao tajwa katika katika mji wa Tehran. 

3488439

Habari zinazohusiana
captcha