Wanaharakati wanaoiunga mkono Palestina waliandamana siku ya Jumanne nje ya hoteli anayoishi waziri wa ulinzi wa Israel, Yoav Gallant wakati wa ziara yake mjini Washington.
“Huwezi kujificha; unafanya mauaji ya halaiki,” waliimba Waandamanaji hao walikuwa na mabango ya kutaka kusitishwa kwa vita huko Gaza na kusitishwa kwa uungaji mkono wa Marekani kwa uvamizi wa Israel.
Wakati Gallant akiwasili kwa mkutano na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken siku ya Jumatatu, waandamanaji walitaka afisa huyo wa Israel akamatwe na kufunguliwa mashtaka kwa mauaji ya kimbari ya raia wa Palestina huko Gaza.
Kabla ya safari yake, Gallant alisema kuwa mikutano yake na maafisa wa utawala wa Biden itajumuisha majadiliano juu ya kuhamia "awamu ya tatu" ya mashambulizi ya Israel huko Gaza, ambayo alielezea kuwa muhimu sana.
Mnamo Oktoba, takriban miezi tisa sas baada ya kuanza kwa uvamizi huko Gaza, Gallant alielezea mpango wa vita wa awamu tatu.
Ilianza na kipindi cha mashambulizi makali ya anga dhidi ya malengo na miundombinu inayodaiwa ya Hamas, ikifuatiwa na kipindi cha kati cha operesheni za ardhini zenye lengo la kuondoa mifuko ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas.
Na pia Kilichofuata ni uharibifu wa miundombinu ya kiraia na kuua au kujeruhiwa kwa Wapalestina zaidi ya 120,000 wengi wao wakiwa wanawake na watoto.
Awamu ya tatu, alisema Gallant wakati huo, itahusisha kuanzisha "ukweli mpya wa usalama" kwa "raia wa Israeli" kwa kufikia malengo yaliyotangazwa ya kuvunja uwezo wa kijeshi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, na uwezo wake wa kutawala huko Gaza.
'Maonyesho' ya Uhalifu wa utawala wa Israeli, Afisa wa Haki Asema
Ni Gallant ambaye alitoa dalili ya wazi ya nia ya Israel ya kufanya mauaji ya halaiki aliposema Oktoba 9 mwaka jana: “Nimeamuru kuzingirwa kabisa kwa Ukanda wa Gaza, Hakutakuwa na umeme, chakula, mafuta, kila kitu kimefungwa."
Mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) anatafuta vibali vya kukamatwa kwa Gallant na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kwa tuhuma zikiwemo za kutumia njaa kama silaha ya vita.
N a Wanakanusha mashtaka hayo Israel pia inashutumiwa kwa mauaji ya halaiki katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ).