IQNA

ICRO ina mpango Unaoitwa Risalatallah ili kuimarisha harakati za Iran za Qur'ani katika Ngazi ya kimataifa

16:21 - July 07, 2024
Habari ID: 3479085
IQNA - Shirika la Iran la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu (ICRO) limebuni mpango unaoitwa Risalatallah ili kuimarisha harakati za Qur'ani za Iran katika ngazi ya kimataifa, afisa mmoja alisema.

Hujat-Al-Islam Seyed Mostafa Hosseini Neyshaburi, Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Qur'ani Tukufu na Uenezi cha ICRO alsema hayo katika mahojiano na Shirika la habari la IQNA na kuongeza kuwa, inasaidia pia kustawisha maelewano kati ya Iran na mataifa mengine ya Kiislamu katika uwanja wa Qur'ani Tukufu.

Alisema hatua tatu za utekelezaji wa mpango huo, ambazo ni tathmini ya uwezo, diplomasia ya Qur'ani na kuunganisha vituo vya Qur'ani, zimekamilika na mipango ya hatua zinazofuata inaendelea. 

Akigusia propaganda hasi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na majaribio ya kueneza fikra potofu kwamba Waislamu wa Shia hawatilii maanani vya kutosha Qur'ani Tukufu, amesema ICRO ikiwa ni kituo cha kiutamaduni cha nchi hiyo nje ya nchi na hasa Kituo chake cha Kimataifa cha Qur'ani Tukufu, wametilia maanani sana kufuta dhana hizo.

Alisema mpango na mkakati wa kina wa Risalatallah umebuniwa kwa msisitizo na rais wa ICRO, Hujat-Al-Islam Mahdi Imanipour.

Inalenga kufikisha jumbe za Qur'ani kwa wale wanaozitafuta na kuunganisha na kuambatanisha uwezo wa Qur'ani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika ngazi ya ndani kwa wale walio nje ya nchi.

Mpango huo pia ni sehemu ya juhudi za kufuata diplomasia ya Qur'ani Tukufu alisema hayo.

Hujat-Al-Islam Hosseini Neyshaburi amebainisha kuwa nyadhifa mbalimbali nchini zikiwemo za watu binafsi, asasi za msingi, taasisi za serikali, wanawake, vyombo vya habari, sanaa za Qur'ani n.k zimetambuliwa na juhudi zimefanyika ili kuzitambulisha katika ngazi ya kimataifa.

Amesema uwezo wa Iran nje ya nchi, wakiwemo mabalozi na maafisa wa kitamaduni umetumika kwa ajili hiyo na diplomasia ya Qur'ani imepewa umuhimu maalum katika diplomasia ya utamaduni wa nchi. 

Khatibu Ahimiza Utafiti kuhusu Diplomasia ya Qur'ani   
Hatua iliyofuata imekuwa harambee na ushirikiano na wengine kwa kuzingatia Qur'ani Tukufu na mazungumzo kwa ajili ya kuendeleza na kufikia malengo ya Qur'ani, aliendelea kusema.

Kumekuwa na uhusiano mzuri ulioanzishwa katika nyanja za kupeleka Qari pamoja na uchapishaji na uchapishaji wa Qur'ani na nchi kama Malaysia, Pakistan, Tunisia na Senegal, alisem

3489030

 

captcha