Wafanya ziyara hawa walitoka Iraq na nchi zingine kushiriki katika hafla ya maombolezo ya Ashura, Al-Alam iliripoti Alhamisi.
Kabla ya hafla hiyo, taasisi za huduma, usalama na afya zilitangaza kufanikiwa kwa mipango yao maalum ya Ashura na maombolezo ya Rakdha Tuwairaj.
Tume ya Mawasiliano na Vyombo vya Habari ya Iraq ilibainisha kuwa waandishi wa habari 725 na kanali 84 za TV ziliangazia taratibu za maombolezo za Ashura mwaka huu.
Zaidi ya hayo, Wizara ya Umeme ya Iraq ilisifu mafanikio ya mpango wao maalum wa Ashura, kuhakikisha usambazaji wa umeme wa saa 24 katika mji wa Karbala.
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Najaf pia uliripoti kupokea zaidi ya wafanya ziyara 71,000 kutoka tarehe 1 hadi 9 ya Muharram.
Muharram 2024: Maombolezo ya Ashura kote Iran katika Picha
Rakdha Tuwairaj ya kila mwaka hufanyika baada ya swala ya Adhuhuri ya Ashura.
Ibada hiyo inaashiria shauku ya watu kumsaidia Imam Hussein (AS), Iraq iliadhimisha Ashura Jumatano, Julai 17, baada ya Ayatollah Mkuu Seyed Ali al-Sistani kutangaza Julai 8 kama siku ya kwanza ya Muharram
Katika nchi nyingine nyingi, Waislamu wa Shia waliadhimisha Ashura siku ya Jumanne.
Rakdha Tuwairaj ni ibada ya siku ya Ashura ambapo waombolezaji hutembea bila viatu kutoka mji wa Hindya (zamani ukiitwa Tuwairaj) karibu na Karbala hadi kwenye madhehebu matukufu ya Imam Hussein (AS) na Hazrat Abbas (AS) huku wakijipiga kichwa na kifua na kisha kuondoka madhehebu ndani ya muda mfupi.
Ni njia ya kufanya upya utii na matarajio ya Ashura. Maombolezo hayo yaliloanzishwa na mtu mashuhuri katika Wilaya ya Hindiya ya Karbala, aitwaye Mirza Salih Qazvini, limekuwa likifanyika kila mwaka kwa takriban miaka 150, isipokuwa wakati ambapo utawala wa Ba’ath wa dikteta wa zamani Saddam Hussein ulitawala Iraq.