IQNA

Harakati za Qur'ani

Zaidi ya Wahifadhi 250 wa Qur’ani wajumuika Ukingo wa Magharibi

23:56 - August 28, 2024
Habari ID: 3479342
IQNA – Kikao cha kuhitimisha Qur’ani kimefanyika huko Nablus, Ukingo wa Magharibi Palestina, wikendi hii iliyopita.

Kuhitimisha Qur’ani au Khatm al-Quran  maana yake ni kusoma Qur’ani Tukufu kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Zaidi ya wahifadhi 250 wakiwemo wanaume, wanawake na watoto walisoma  Qur’ani  katika hafla hiyo, kwa mujibu wa gazeti la kila siku la Al-Arabi al-Jadid.

Huu ulikuwa ni mpango wa kwanza wa Qur'ani kama huu kuandaliwa katika Ukingo wa Magharibi.

Washiriki walianza kusoma Quran baada ya sala ya asubuhi na kuhitimisha Magharibi.

Kikao hicho kiliandaliwa  na Kamati ya Kuhifadhi Qur'ani ya Nablus, ambayo ina wanachama zaidi ya 500.

Shughuli za Qur'ani hazijapungua katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan licha ya ghasia za walowezi wa Kizayuni wa Israel ambapo  takriban kila siku Wazayuni wakipata himaya ya jeshi la utawala huo ghasibu  huvamia miji na vijiji.

3489679

captcha