Hayo yamedokezwa na Katibu mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu (WPIST) katika mkutano na waandishi wa habari Jumamosi asubuhi ameongeza kuwa Rais Masoud Pezeshkian atahutubu katika ufunguzi wa kongamano hilo.
Hujjatul-Islam Hamid Shahriari amesema mada ya mkutano wa mwaka huu ni "ushirikiano wa Kiislamu kwa ajili ya kufikia maadili ya pamoja kwa kuzingatia suala la Palestina".
Aidha amedokeza kuwa udugu wa Kiislamu na kuepuka fitna na migogoro ni miongoni mwa maadili yatakayosisitizwa katika mkutano huo..
Jumla ya wasomi 234, wanafikra na wanazuoni wa Kiislamu, kitamaduni na kisiasa watahutubia mkutano huo.
Kutakuwa na wageni kutoka nchi 30 za Kiislamu, zikiwemo Saudi Arabia, Jordan na Umoja wa Falme za Kiarabu, pamoja na nchi nyingine kama Marekani na Russia.
Hujjatul-Islam Hamid Shahriari ameongeza kuwa vitabu 12 vipya vitazinduliwa katika sherehe wakati wa hafla hiyo ya kimataifa.
Siku ya Jumapili, Septemba 21, ambayo ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) na Imam Sadiq (AS), washiriki wa mkutano huo watakutana na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyed Ali Khamenei, alisema.
Hujjatul-Islam Hamid Shahriari aliendelea kusema kwamba mkutano huo utakamilika kwa taarifa ya mwisho mnamo Septemba 21.
Siku ya 17 ya Rabiul Awwal, ambayo ni Septemba 21 mwaka huu, inaaminika na Waislamu wa madhehebu ya Shia kuwa siku ya kukumbuka kuzaliwa kwa Mtume Mohammad (SAW), wakati Waislamu wa Sunni wanaamini tarehe sahihi ni 12 Rabiul Awwal
Muda kati ya tarehe hizo mbili huadhimishwa kila mwaka kama Wiki ya Umoja wa Kiislamu.
Hayati Mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Imam Khomeini (RA) ndiye alitangaza muda baina ya tarehe hizo mbili kuwa Wiki ya Umoja wa Kiislamu nyuma katika miaka ya 1980.
3489891