IQNA

Qurni Tukufu

Mkuu wa Al-Azhar: Miujiza ya Kisayansi ya Qur'ani Tukufu Inawashangaza Wanasayansi

20:08 - October 16, 2024
Habari ID: 3479601
IQNA - Rais wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri alisema Qur'ani Tukufu ina miujiza mingi ya kisayansi ambayo imewashangaza wanasayansi katika nyanja tofauti.

Dkt. Salama Dawood alisema marejeo ya kimiujiza ya Qur'ani kwa ukweli wa kisayansi yanaonyesha ukuu wa Muumba.

Alisema kuna miujiza mingi katika aya za Qur'ani ikiwemo inayohusiana na namba, Tashriee (sheria) na sayansi.

Kwa mfano, alirejea Aya ya 88 ya Surah An-Naml inayoangazia mwendo wa milima: “Na unaiona milima unaidhunia imetulia; nayo inakwenda kama mwendo wa mawingu. Huo ndio ufundi wa Mwenyezi Mungu aliye tengeneza vilivyo kila kitu. Hakika Yeye anazo khabari za yote myatendayo.”

Nyingine, akasema, ni Aya ya 40 ya Sura An-Nur inayozungumzia giza ndani ya moyo wa tazama, “Au ni kama giza katika bahari kuu, iliyo funikwa na mawimbi juu ya mawimbi, na juu yake yapo mawingu. Giza juu ya giza. Akiutoa mtu mkono wake anakaribia asiuone. Na ambaye Mwenyezi Mungu hakumjaalia kuwa na nuru hawi na nuru.”

Marejeleo ya hatua za ukuaji wa kijusi (Aya ya 13 ya Surah Al-Muminoun), mzunguko wa maji (Aya ya 48 ya Surah Al-Furqan), na jukumu la milima na bahari katika kuleta usawa duniani (Aya ya 30 ya Surah Al-Anbiya) , ilikuwa miongoni mwa mifano mingine ya miujiza ya kisayansi ya Qur'ani Tukufu ambayo mkuu wa Al-Azhar aliangazia.

Vile vile amesisitiza haja ya kuongeza ufahamu kuhusu umuhimu wa utafiti wa kisayansi wa Qur'ani.

 

4242382

captcha