IQNA

Miujiza ya Qur'ani

Mkutano wa Misri: Miujiza ya Kisayansi ya Qur'ani imethibitishwa na sayansi ya kisasa

15:27 - October 27, 2024
Habari ID: 3479652
IQNA - Wanachuoni na wanafikra waliohudhuria mkutano huko Cairo juu ya miujiza ya kisayansi ya Qur'ani na Sunnah wamesitiza kwamba miujiza ya kisayansi ya Qur'ani Tukkufu imethibitishwa na sayansi ya kisasa.

Miujiza ya kisayansi katika Qur'ani na Sunnah inazungumza na watu kwa lugha ya sayansi, wamesema.
Mkutano huo umeandaliwa katika mji mkuu wa Misri na Jumuiya ya Miujiza ya Qur'ani na Sunnah ya nchi hiyo chini ya usimamizi wa Chuo Kikuu cha Al-Azhar.
Abdullah bin Abdul Aziz Muslih, ambaye ni rais wa heshima wa jamii, alisema katika hotuba yake katika mkutano huo kwamba mambo ya kisayansi yaliyogunduliwa katika zama za kisasa yanathibitisha miujiza ya kisayansi ya Qur'ani.
Ameongeza kuwa, Kitabu kitukufu kinahutubia watu kwa lugha ya mantiki na akili.
Ali Fuad Mukhaimir, rais wa mkutano huo amesema kuna dalili na marejeo mengi ya ukweli wa kisayansi ndani ya Qur'ani Tukufu, nyingi kati ya hizo zimegunduliwa hivi karibuni tu na sayansi ya kisasa.
Qur'ani, iliyoteremshwa karne 14 zilizopita, imekuwa mwanzilishi katika ugunduzi wa ukweli wa kisayansi, alisema.
Miujiza ya kisayansi ya Qur'ani inashughulikia mada mbali mbali, kuanzia uumbaji wa mimea, ndege, wadudu na wanyama wengine hadi dawa, miujiza ya balagha n.k, Mukhaimir aliendelea kusema.
Amesisitiza ulazima wa kutumia sayansi na akili kujibu mashaka na maswali yanayoibuliwa na maadui wa Uislamu kwa lengo la kudhoofisha imani ya vijana wa Kiislamu.
Vile vile amebainisha kuwa mkutano huo unalenga kuangazia vipengele mbalimbali vya miujiza ya kisayansi ya Qur'ani Tukufu na Sunnah na kujadili kuanzishwa kwa mradi wa kuandaa ensaiklopidia ya istilahi zinazohusiana na miujiza ya kisayansi ya Qur'an na Sunnah.
Mkutano huo wa siku mbili ulioanza Jumamosi, unaangazia uwasilishaji wa karatasi 21 za utafiti.

3490439

captcha