IQNA

Warsha ya Qur’ani Katika Msikiti wa Mtume yalenga kukuza utaalamu wa Qira’at

21:00 - July 23, 2025
Habari ID: 3480987
IQNA – Warsha ya mafunzo kuhusu misingi ya Qira’at kumi za Qur’ani Tukufu imezinduliwa katika Msikiti wa Mtume (SAW) - Al Masjid an Nabawi, mjini Madina, Saudi Arabia.

Uongozi wa Masuala ya Kidini wa Msikiti Mtakatifu wa Makka na Al Masjid An Nabawi au Msikiti wa Mtume (SAW), kupitia Idara ya Miduara ya Qur’ani Tukufu na Mutoon, umetangaza uzinduzi wa warsha hii kama sehemu ya programu zake za kielimu kwa lengo la kueneza elimu ya Qur’ani na kukuza utaalamu maalumu katika fani ya Qira’at.

Warsha hiyo ilianza rasmi tarehe 21 Julai 2025, na itafanyika kila siku ya Jumatatu baada ya Swala ya ‘Isha katika Msikiti wa Mtume (SAW). Washiriki watakaohudhuria kwa ukamilifu watapewa cheti rasmi cha ushiriki kilichothibitishwa na uongozi husika.

Uongozi huo umealika wale wote wenye hamu na mapenzi ya kujifunza Qira’at na elimu ya Qur’ani kufuatilia akaunti rasmi za mitandao ya kijamii ili kupata taarifa za usajili.

3493950

Habari zinazohusiana
captcha