IQNA

WHO: Madina ni miongoni mwa miji yenye hali bora zaidi ya afya duniani

12:29 - January 28, 2021
Habari ID: 3473599
TEHRAN (IQNA) – Shirika la Afya Duniani limeutangaza mji mtakatifu wa Madina kuwa miongoni mwa miji yenye hali bora zaidi ya afya duniani.

WHO imetoa tathmini hiyo baada ya ujumbe wake kuutembelea mji huo na kubaini kuwa una vigezo vyote vya kimataifa vya kutambuliwa kuwa mji wenye huduma bora za afya.

Inaaminika kuwa mji wa Madina ni kwa kwanza wenye idadi ya watu zaidi ya milioni mbili ambao umepata hadi ya kuwa  'mji wenye afya bora.'

Mashirika 22 ya kiserikali, kijamii, ya kutoa misaada na ya watu wenye kujitolea yalisaidia WHO katika mchakato kutathmini hali ya huduma na suhula za afya mjini humo.

Kwa mujibu wa WHO, 'mji wenye afya bora' ni mji ambao daima huchukua hatua za kubuni na kuboresha mioundomsingi na mazingira ya kijamii sambamba na kuiwezesha jamii kusaidiana katika kutekeleza majukumu yote ya kimaisha na kufikia uwezo wa juu kabisa.

Mji wa Madina uko kaskazini mwa Riyadh, mji mkuu wa Saudi Arabia kati kati mwa Najd na ni mji wenye hali ya hewa kavu na joto kali na pia baridi kali wakati wa msimu wa baridi. Jina la mji huo lilikuwa ni Yathrib kabla ya Hijra ya Mtume Muhammad SAW na ulijulikana kama Madina al Nabii (Mji wa wa Nabii) baada ya kuwasili Mtume Muhammad SAW. Msikiti wa Mtume SAW, Al-Masjid an-Nabawi, Msikiti wa Quba na Msikiti wa Qibalatian ni misikiti muhimu iliyo katika mji huo. 

3950420

Kishikizo: madina WHO
captcha