IQNA

Habari za Madina

Waliofika Msikiti wa Mtume (SAW) Madina wapokea chupa milioni 2.2 za maji ya Zamzam ndani ya Miezi 3

17:59 - November 25, 2022
Habari ID: 3476144
TEHRAN (IQNA) - Zaidi ya chupa milioni 2.2 za maji ya Zamzam ziligawiwa waumini waliofika katika Msikiti wa Mtume (Al-Masjid an-Nabawi) huko Madina katika robo ya kwanza ya mwaka huu wa Hijri.

Idara ya  Urais wa Masuala ya Misikiti Miwili Mitakatifu umetoa katika robo ya kwanza ya mwaka huu wa Hijri zaidi ya tani 15,000 za maji zilizopokelewa kupitia matangi.

Jumla ya maji yaliyotumiwa katika robo ya kwanza yalifikia tani 13,128, wakati idadi ya vibuyu vya maji vilifika 494,508 na chupa zilizosambazwa za maji ya Zamzam zilifikia zaidi ya 2,265,128, kulingana na takwimu zilizotolewa na idara hiyo.

Halikadhaila idara hiyo huzingatia kwa kina suala la kupima mahali pa kujazia maji na huchukua sampuli mara kwa mara ili kuhakikisha usalama wa maji, ambapo idadi ya sampuli zilizojaribiwa ilifikia karibu sampuli 4,470.

3481388

Kishikizo: zamzam ، maji ، al masjid an nabawi ، madina
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha