IQNA

Taarifa

Baraza la Usalama lalaani hujuma ya kigaidi la dhidi ya maafisa wa polisi nchini Iran

21:36 - October 31, 2024
Habari ID: 3479676
IQNA-Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesikitishwa na shambulizi la kigaidi la Jumamosi dhidi ya msafara wa polisi katika Mkoa wa Sistan na Baluchestan kusini mashariki mwa Iran ambapo maafisa 10 wa polisi waliuawa shahidi.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana Jumatano, chombo hicho chenye wanachama 15 "kililaani vikali" shambulio la "kigaidi la woga dhidi ya kitengo cha doria cha Kamandi ya Polisi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mkoa wa Goharkooh wa mji wa Taftan. "

Taarifa hiyo pia ilitoa pole nyingi na rambirambi kwa familia zilizofiwa, pamoja na watu wa Iran na serikali kufuatia msiba huo.

Hali kadhalika taarifa hiyo imesema: "Wanachama wa Baraza la Usalama wamesisitiza haja ya kuwawajibisha wahalifu, waandaaji, wafadhili na waungaji mkono wa vitendo hivi vya kulaumiwa vya ugaidi na kuwafikisha mahakamani."

Wanachama wa Baraza la Usalama wametaka mataifa yote, kwa mujibu wa majukumu yao chini ya sheria ya kimataifa na maazimio husika ya Baraza la Usalama, kushirikiana kikamilifu na Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, pamoja na mamlaka nyingine zote zinazohusika katika suala hili.

Wakati huo huo, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesisitiza kuwa, ugaidi wa aina zote na madhihirisho yake ni moja ya vitisho vikali zaidi kwa amani na usalama wa kimataifa, na kwamba vitendo vyovyote vya ugaidi ni jinai na havikubaliki.

Kikundi cha kigaidi kinachojiita Jaish al-Adl kilidai kuhusika na shambulio hilo la kuvizia dhidi ya msafara wa magari ya polisi ya Iran.

Kikundi hicho cha magaidi kinachoungwa mkono na mataifa ya kigeni, chenye makao yake nchini Pakistan, kimehusika katika mashambulizi mengi yanayolenga raia na vikosi vya usalama katika mkoa wa mpaka wa Sistan na Baluchestan katika miaka kadhaa iliyopita

 

4245389

captcha