IQNA

Mawaidha

Mtazamo wa Uislamu kuhusu michezo

15:15 - November 23, 2024
Habari ID: 3479793
IQNA - Katika Uislamu, kushiriki katika michezo kwa nia safi au ikhlasi hubadilisha shughuli za kimwili kuwa tendo la ibada, kukuza afya ya kimwili na ustawi wa kiroho.

Haya ni kwa mujibu wa Ayatullah Ahmad Moballeghi, mwanazuoni mwandamizi wa Uislamu nchini Iran ambaye pia ni mhadhiri katika vyuo vikuu vya Kiislamu (Hauza). Ametoa kuali hiyo katika Makala iliyochapishwa kwa lugha ya katika Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA. Ifuatayo ni sehemu ya makala hiyo.
Michezo inaotokana na maumbile asili ya binadamu. Hamu ya michezo imekuwa ikitiririka katika mishipa ya jamii tangu mwanzo wa wakati, bila kujali rangi na lugha zao mbalimbali.
Ukweli huu unathibitisha mfanano wa kimsingi miongoni mwa wanadamu: msukumo wa kisilika wa pamoja wa harakati, nguvu, uratibu, na ushindani—msukumo ambao umevuka mipaka ya wakati na eneo na kuonyesha nukta ya pamoja ya wanadamu.
Katika Uislamu, michezo inaweza kuchunguzwa kupitia kanuni kadhaa za msingi: nguvu, kuzingatia shughuli za manufaa, mlingano, ushindani katika wema, na ibada ikiwa kuna nia safi..
Kuhusu kanuni ya nguvu ya kimwili na kiroho, Mtume Muhammad (SAW) alisema: “Muumini mwenye nguvu ni bora na anapendwa zaidi na Mwenyezi Mungu kuliko Muumini dhaifu." Mwili wenye afya huleta nguvu na uwezo, wakati mwili mgonjwa au dhaifu husababisha udhaifu na kutokuwa na utulivu.
Vivyo hivyo, nafsi, kama mwili, ikiwa na afya nzuri, huangaza nguvu na uchangamfu, lakini inapofadhaika au kuumwa, hushindwa na kukata tamaa. Hivyo basi, ustawi wa kimwili na kiakili ni ufunguo wa nguvu ambayo Uislamu unaitaka.
Kuhusiana na kuzingatia mambo ya manufaa, Mtume (SAW) alishauri: “Kuwa makini na nini kinakunufaisha.” Michezo, ina hazina ya manufaa na  inakuza afya ya kimwili, mlingano kisaikolojia, na umoja wa jamii.
Mwili wenye nguvu, kupitia mchezo, unakuwa chombo cha ibada na matendo mema, nafsi yenye mlingano  huepuka kufurutu ada, na jamii yenye maelewano hukuza mshikamano na ushirikiano chini ya mwavuli wa michezo.
Michezo si shughuli ya kupita tu; ni ujumbe wa milele unaonong'oneza ubinadamu: "Uwe hodari katika mwili, waungwana katika roho, na uwe na manufaa kwa jamii yako."
Kwa kanuni ya mlingano, Uislamu, kama dini ya wastani, unawaita wanadamu kuwa na mtazamo wa wastani katika nyanja zote za maisha. Moja ya maonyesho ya wazi ya usawa huu ni maelewano kati ya mwili na roho.
Mchezo hupumua maisha ndani ya roho, huondoa wasiwasi, na huleta utulivu, huwezesha sio mwili tu bali pia roho. Inaweza kufagia huzuni, hasa ikiambatana na ukumbusho wa Mwenyezi Mungu yaani Dhikri, na pia ni chanzo cha nguvu na uwezo.
Kuhusu ushindani katika wema, Qur'ani Tukufu inasema: “Na kila mmoja anao upande anao elekea. Basi shindanieni mema. Popote mlipo Mwenyezi Mungu atakuleteni nyote pamoja. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.” (Sura Al-Baqarah, aya ya 148).
Kutazama mchezo kupitia lenzi ya faida na wema, mashindano ya michezo mbali mbali yanaweza kujumuisha wito huu wa Mwenyezi Mungu. Ushindani katika michezo sio tu unakuza ukuaji wa mtu binafsi bali pia huimarisha roho ya umoja na ushirikiano ndani ya jamii.
Ama Ibada kwa nia ya ikhlasi, inasemekana kwamba matendo yote yanahukumiwa kwa nia zao. Ikiwa mtu atashiriki katika mchezo kwa moyo safi na kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu, harakati za kimwili hubadilika na kuwa vitendo vya Dhikri, na juhudi hii inakuwa aina ya ibada.

3490784

captcha