IQNA

Wanariadha Waislamu

Mwanamke Muirani abusu Msahafu, asujudu baada ya kushinda dhahabu katika Michezo ya Olimpiki ya Walemavu

23:14 - September 01, 2024
Habari ID: 3479365
IQNA – Mwanamke Muirani Sareh Javanmardi wa Iran ameubusu Msahafu (nakala ya Qur'ani Tukufu) baada ya kushinda medali ya dhahabu katika mashindano ya Olimpiki ya Walemavu 2024 huko Paris, hatua ambayo imewavutia Waislamu duniani kote na kupongezwa na  taasisi kuu ya Qur'ani.

Javanmardi, mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Irna,  alipata medali ya dhahabu katika mashindano ya kufyatua bastola ya kategoria ya 10m Air Pistol SH1 katika Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya 2024 huko Paris.

Siku ya Jumamosi, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 39, ambaye awali alishinda dhahabu kwenye Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Tokyo 2020 na Rio 2016, alijizolea pointi 236.8 na kutwaa nafasi ya kwanza. Mwakilishi wa Uturuki Aysel Ozgan alipata medali ya fedha kwa pointi 231.1, huku mwanariadha wa India Rubina Francis akitwaa shaba kwa jumla ya pointi 211.1.

Mara tu baada ya kushinda, alibusu nakala ya Qur’ani Tukufu kabla ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kusujudu juu ya bendera ya Iran.

Mkuu wa Taasisi ya Dar-ul-Quran ya Iran ametoa taarifa na kusifu hatua ya mwanariadha huyo katika kuheshimu Qur'ani Tukufu.

"Ni chanzo cha fahari na heshima kwamba mwanamke wa Kiislamu anang'aa katika nafasi hiyo, na katika kilele cha uzuri wake, anaionyesha Qur’ani Tukufu kama bendera ya ubinadamu wake pamoja na kuienzi bendera yake ya kitaifa mbele ya walimwengu," Hujjatul Ali Taqizadeh aliandika katika taarifa ya Jumapili.

“Kitendo hiki cha shujaa huyu wa kitaifa mwenye ustahiki kilionyesha kwamba, katika mazingira ambayo Shetani na majeshi yake wamewalenga wanawake na familia bila kuchoka, wakilenga kuwanyima wanawake baraka za umama, mke na utulivu wa maisha ya familia kupitia kauli mbiu za udanganyifu. uwepo wa mwanamke kama huyo kwa hakika ni baraka ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu; kitabu ambacho kinaendelea kuuvisha mwili na roho vazi la uchamungu, kikipamba ubinadamu na ushujaa wake machoni pa watazamaji bila kujali umbile lake au jinsia yake,” aliongeza.

3489733

captcha