IQNA

Mavazi ya michezo ya wanawake Waislamu

14:41 - June 13, 2015
Habari ID: 3313760
Kwa msaada wa Chuo Kikuu cha Minnesota Marekani, wasichana Waislamu katika eneo la Minneapolis wamebuni mavazi mapya ya timu yao ya baskatboli, mavazi ambayo yanazingatia mipaka ya Kiislamu.

“Sikuwa naweza kutekeleza harakati katika uwanja wa michezo kwa sababu ya kuvaa sketi na nilikuwa naanguka mara kwa mara,” amesema  Sihal Ali, mchezaji Mwislamu katika timu ya basketboli ya Cedar-Riverside.
Matatizo hayo yalimalizika pale mavazi mapya ya wasichana Waislamu yalipobuniwa na Taasisi ya Mitindo ya Nguo ya Chuo Kikuu cha Minnesota kwa ushirikiano na Kituo cha Utafiti cha Tucker kuhusu Wasichana na Wanawake katika Michezo.
Wachezaji waliotumia mavazi hayo wamebainisha kurudhika kwao kwani wanaweza kujihusisha katika michezo na wakati huo huo kujistiri na kuzingatia hijabu ya mwanamke Mwislamu.
Kuna takribani Waislamu milioni nane nchini Marekani na wamekuwa wakijitahidi kulinda utambulisho wao wa kidini pamoja na kuwepo  changamoto nyingi katika nchi hiyo.../mh

3313552

captcha