IQNA

Swala

Watu wa Jordan washiriki Swala ya  Istisqa huku kukiwa ukame wa muda mrefu

20:22 - November 25, 2024
Habari ID: 3479805
IQNA – Wakikabiliwa na kuchelewa kwa mvua kunyesha, wananchi wa Jordan walikusanyika katika misikiti kote nchini kutekeleza Swala ya Al-Istisqa (Swala ya Kuomba Mvua), wakiomba rehema za Mwenyezi Mungu ikiwa ni katika kufuata Sunna ya Mtume Muhammad (SAW).

Maombi hayo yalileta umati mkubwa wa watu katika misikiti kote nchini siku ya Jumapili. Katika Mji wa Al-Hussein, Swala ya Jamaa iliswalishwa na Waziri wa Wakfu, Masuala ya Kiislamu, na Maeneo Matakatifu, Mohammad Al-Khalayleh na kushirikisha Mufti Mkuu wa Jordan Ahmad Al-Hasanat na waumini wengi.

Al-Khalayleh alitoa khutba yenye kuwataka waumini kumwendea Mwenyezi Mungu kwa ikhlasi na unyenyekevu, wakitafuta rehema zake kwa ajili ya ustawi wa watu, mimea na wanyama.

Alitilia mkazo umuhimu wa kiroho wa kuepuka dhambi, ambazo, alisema, mara nyingi huonwa kuwa vizuizi kwa baraka za kimungu kama vile mvua.

3490812

Kishikizo: Istisqa swala
captcha