Kwa mujibu wa tovuti ya akhbaar24, Abdullah mwenye umri wa miaka 9 ana asili ya Bangladesh.
Amehifadhi Qur'ani kikamilifu na ameweza kupata alama nzuri katika mitihani ya kuhifadhi kitabu hicho kitakatifu katika Taasisi ya Kuhifadhi Qur'ani ya Khayrukum mjini humo.
Baba yake amesema Abdullah alianza kuhifadhi Qur'ani katika Msikiti wa al-Rajih mjini humo miaka miwili iliyopita.
Abdullah amekuwa akihifadhi kurasa mbili za Qu'rani kila siku na kwa msingi huo aliweza kuhifadhi Qur'ani kwa muda mfupi sana.
Abdullah anasema anapenda kuwa mwanazuoni wa kidini ili aweze kuwasaidia watu katika masuala ya Kiislamu.
Abdullah ni kati ya wavulana na wasichana 1,000 waliohifadhi.